Huu ndio ukweli mchungu kuhusu katiba mpya, mh rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Huu ndio ukweli mchungu kuhusu katiba mpya, mh rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Posts
4,879
Reaction score
1,126
Mh rais wa jamhuru ya muungano ya tanzania nikiwa kama mtanzania ninalo jukumu na deni kwa nchi yangu na watu wake kushiriki kwa namna moja au nyingine kushiriki katika mchakato unaoendelea nchini mwetu wa kupata katiba mpya,nikupongrze kwa uamuzi wako uliouchukua wa kulikubali wazo la kuanzisha mchakato japo ndani ya chama chako ilikuwa haikubaliki sirini na hadharani.

Mh rais viongozi waandamizi ndani ya chama chako waliwahi kukaririwa wakidai hakuna haja ya katiba mpya na wala serikali haina pesa za kugharimia katiba hivyo iliyopo inatosha.haohao ndio ulioshirikiana nao kuandaa mchakato na hatimaye umewafanya kuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba.mh rais naomba niwe nabii kwa muda wa kutabiri nkuwa tanzania haitapata katiba mpya na tukipata tukakachokiita ni katiba mpya nikuambie kabisa kuwa itadumu kwa miaka miwili tu mpaka january 2016 tutakuwa tunahitaji katiba mpya kwani hii itakuwa imemaliza kazi yake kwani imelenga uchaguzi wa serikali za mitaa(japo haittataja hizo serikali)na uchaguzi mkuu 2015.

Mh rais kutokana na mihangaiko yangu jana nilipata nafasi ya kusikiliza bunge maalum la katiba katika kipengele cha kuchangia rasimu ya kanuni na nilipata bahati ya kuwasikiliza makada wa chama chako wafuatao,jumanne maghembe,zaakia meghji,livingstone lusinde,peter serukamba na wanasiasa kutoka vyama vingine kama ezekiah wenje,mzee cheyo,james mbatia,moses machali lipumba na baadhi kutoka zanzibar.

Mh rais uliamua kuukwamisha huu mchakato kwa nkuamua kuwaleta wabunge wa bunge la muungano na baraza la wawakilishi ili kukifaidisha chama chako lakini kosa hili hutakaa ulisahau,wabunge malengo yao yanafahamika,idadi yao inafahamika,waliokushauri kuhusu idadi ya wajumbe wa kuteuliwa na wewe baada ya majina yao kupendekezwa kwako walishaliona hili,idadi ya wana siasa katika bunge maalum la katiba kuwa 90% ni kosa,ni kukubali kushindwa kabla ya kuanza,wana siasa ni wataalamu wa propaganda na uongo,umajua hawa wanaweza kukuahidi daraja hata kama huna mto na kwa maneno matamu ukawapa kura na baada ya muda ndio ukagundua huna mto na tayari umesha mchagua.

Mh rais katiba mpya haihitaji propaganda wala ushawishi wa kampeni.ni maisha ya watu,ni hatma ya nchi yao na vizazi vyao.

Mh rais ccm ina wanachama milioni kama tano,chadema kama mbili,cuf,nccr na wengineo kama moja hivi kwa hiyo kwa watanzania milioni 45 kuwakilishwa na 90%ya watu milioni nane hii sio haki kabisa wale miloni 37 wanawakilishwa na nani?

Mh rais nani asiyemjua kingunge ngombale mwiru na misimamo yake?nani asiyejua kuwa ni mwanasiasa 101%?kwa nini ulimchagua kupitia asasi ile?nani alikushauri vile?je ni chikawe au kombani?mh rais ccm walistahili kihaki kuwa na wawakilishi 10% tu kutokana na wanachama wao milioni5 walionao nchini na chadema 5% vyama vingine 3% makundi mengine 72% hapo tungepata katiba nzuri na yenye focus ya miaka hata zaidi ya 100 ijayo.

mh rais wakati wa kukabidhiwa rasimu ya pili nilikusikiliza hotuba yako ilikuwa nzuri ya kuonya,kushauri na kuelekeza ni nini cha kufanya ili kupata katiba mpya,chama chako hakikutaka kukusikiliza kimejiandaa kupambana mpaka kitimize lengo la kukwamisha kiu ya watanzania kwa gharama za watanznia.

Mh rais dhamira ya ccm ni kupata katiba wanayoitaka wao au ikishindikana kurudi katika katiba ya zamani bila kujali gharama zilizotumika,na ninayasema haya kwa ujasiri mkubwa kwani yanaonekana kwenye nyuso zao,midomo yao na vifua vyao,mh rais kanuni za bunge zinakataza kujirekebishia kanuni wakati mkiwa bungeni hili lilifanywa makusudi ili kuondoa dhana ya kujipendelea,bunge maalum la katiba lilitakiwa kuondoa haya,wanasiasa siku zote ni watu wa kujipendelea,angalia suala la posho,mh ndasa anajua kuwa yeye ni mbunge na ana mshahara,ana mafuta ya gari kila mwezi,ni mjumbe wa kamati na inawezekana ni mjumbe wa bodi wa shirika flani.anajua uwezo wa serikali yako kimapato,anajua ukubwa wa deni la taifa anajivika upofu,anajilinganisha na mweta kutoka songea?

Mh rais nisingpenda kukushauri ulivunje hili bunge ila nategemea kwa busara yako utafikiria mara mbili kuhusu watu wanaofaa au njia bora ya kulipatia taifa hili katiba bora na mpya,najua unajiandaa kuungana na marais wastaafu na kubaki na hesshima ya kutukuka ya kusimamia na kuandaa katiba bora,usife moyo nakutia shime umekula ng'ombe 80% kilichobaki ni kidogo lakini muhimu kuliko ulichokwisha kukifanya,hii ni penati inayoenda kumaliza mchezo,macho nya watanzania iko kwako,ni kama macho ya waitalia kwa roberto baggio mwaka 90.

kina chenge hawana usafi wa kututungia katiba,wameanza kuibiana simu.

naomba utafakari tena mh rais.

nawakilisha haya pamoja na kuwa ninayo mengi kuhusu hilo.
 
Kati ya mambo ambayo nlidhani watanzania tutaweza kwenye hili lakini tumelianza ovyo kweli...hivi sisi watanzania tunaweza nini..? Inasikitisha
 
dr.mo tunachokiweza nafikiri ni ngono na majungu vitu ambavyo havihitaji kutumia akili.
 
Ni kweli tupu uliyosema ,hili bunge la katiba limekalia kiushindani wa kisiasa na limevutwa zaidi kwenye upande wa CCM na hii imeshaanza kuonekana mvutano ,mvutano na halipo kutafakari maslahi ya Nchi na kuweka muelekeo mzuri.

Bunge limejaa UCCM ,hebu ulizia viongozi wa kamati zilizoundwa wa bunge hilo utaona ,japo Raisi alisema wajumbe wote wanatokea au ni wapenzi wa vyama vya siasa kama alitambua hivyo kwa nini hakutafuta uwiano unaokaribiana ?

Isipokuwa kinachotarajiwa ni kwa wajumbe mashujaa kuwa wajasiri na kukata mzizi wa fitna kuyakubali yale wanayoyataka baadhi ya wakuu wa chama hicho ambayo wanataka kuyalazimisha kwa maslahi binafsi na yale ambayo wanataka kuyalazimisha japo wananchi walio wengi wameyatolea maoni yao na wao vigogoccm kuona yanahatarisha uwepo wao ,angalia wanavyolazimisha serikali mbili ,kwamba ni lazima hata kufika kuchapisha rasimu yao na kuisambaza kinyemela.

Inakubalika kila chama kina maoni yake lakini na si kuwakilisha rasimu hapa ccm inataka kutumia udikteta kwamba katika chama chao hakuna kupinga serikali mbili japo imebainika wengi wao ndani ya ccm wajumbe wasiokuwa na ubavu hawakubaliani na matakwa ya serikali mbili na wanahoji inakuwaje tutake serikali mbili halafu tuwe na Baraza la wawakilishi la Tanganyika(wameibatiza na kuiita Tanzania Bara) kwamba vigogoccm wameshindwa wanashindwa hata kuitamka Tanganyika kutoka kwenye vinywa vyao na maandiko yao , kwa nini imefikia hivyo ?
 
dr.mo tunachokiweza nafikiri ni ngono na majungu vitu ambavyo havihitaji kutumia akili.
hata ngono hatuwezi wewe hujawahi kuangalia mikanda ya wenzetu wanavyoshughulika utadhani wanagombana kumbe wanapeana raha.
 
Kweli katka hili ccm wanaudhi. Wangewaachia waliyoihitaji katiba mpya ndiyo waweze kumshauri huyu Fastjet.
 
kitu cha msingi hao ma ccm wanatakiwa kuelewa katiba si siasa, wakisha fanya katiba kuwa siasa basi wajue wanalea ugonjwa au jipu likitumbuka maumivu yake yatakuwa makali kuliko au tiba yake itakuwa na consequences kubwa, na hao wajumbe waelewe wengi wao in 5 yrs to 10 hawata kuwepo kwenye system au siasa, wakati hiyo katiba itaweza kuendelea kuwepo na hayo mapungufu.
 
Ubinafsi ndo tatizo kubwa la viongozi wetu hapo wanachowaza ni madaraka tu,na kusahau maslahi ya mamilioni ya watanzania!na baya zaidi wanafikiri wataishi miaka mia!ila wakae wakijua wanacheza na muda wakati ukifika kwa watanzania kupata katiba mpya hakuna atakayeweza kuzuia.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom