Huu ndio ukweli wa namna ya kufanikiwa na kupata utajiri mkubwa

Huu ndio ukweli wa namna ya kufanikiwa na kupata utajiri mkubwa

stakehigh

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
7,134
Reaction score
4,556
Katika moja ya matamanio ya wana dunia wengi ni kupata mafanikio makubwa katika upande wa kifedha, hivo husababisha watu kujaribu kutumia njia nyingi sana ili kuongeza nafasi zao za kufikia utajiri huo, lakini ukwel wa utajiri umejificha katika sehem ndogo sana

Mimi sio tajiri lakini nlipofikia sio haba, japo pia nna safari kufika sehem husika! katika ruka ruka zangu za maisha na kukutana na watu wenye mafanikio ya kifedha naweza sema utajiri unatokana na BAHATI,

Najua ni kituko kusema ivo ila utajiri hautafutwi bali ni combination ya mda na wewe umejiandaa vp, leo hii matajiri wote wa dunia tukichukua fedha zao zote na kuwaambia waaanze upya basi ni asilimia ndogo sana itarudi kwenye utajiri, huenda ata anaweza asirudi ata mmoja!

Kuna story nyingi sana za watu kupata utajiri kwa nguvu za giza,, sijawahi kuthibitisha lakini kama ni kwel wapo basi watakua exceptional na sizungumzii kundi hili, kundi linalozungumziwa apa ni kundi la waliofanikiwa kwa kua na biashara ama nafasi kubwa za kiofisi, haswa haswa upande wa biashara!

Naweza kusema matajiri asilimia kubwa walipata utajiri wao bila wao kujua watakuja kua matajiri, ilitokea tu huduma yao ilifanikiwa kufika watu wengi zaidi, ni ajabu kuona watu wakiwa wanautafuta utajiri kwa nguvu sana karne hii

japokua utajiri pia ni bahati lakini huambatana na juhudi, juhudi zinapokutana na bahati ndipo utajiri huzaliwa
 
.....naamini hivyo pia mkuu.
Kuna watu wanapambana sana usiku na mchana wanafikia hata kwenda kwa waganga na kuua ndugu na jamaa zao lakn hola...ila wengine kila kitu akigusa kinaenda.
 
Utajiri sio juhudi na bahati pekee kuna vingi zaidi
Hivi ukiangalia Top 100 ya matajiri duniani unajifunza nini?
1.Wengi umri umeenda,kwahiyo utajiri unahitaji muda kuutengeneza.
2.Wengi wana Story ndefu ya kuanguka na kusimama kwenye biashara, sio rahisi kuna shule chungu kwa vitendo ila hawakati Tamaa wana imani kali.
3.Sio kila biashara inaweza kukupa utajiri (Understand and follow the right path)
4.Usiogope kutake risk, wewe mwajiriwa unayetamani kuwa tajiri lakini unaogopa kuacha ajira ili ujikite kwny vitu vyako unategemea muuujiza?, sio bahati nakataa
5.Akili isilale ujue kubadilika na nyakati kwenye biashara na uwekezaji, kuna ushindani Mpya sokoni, teknolojia mpya,sheria kubadilika so usiwe rigid
 
1) umri sio kigezo wakina bilgates, zakabag walipata utajiri mapema sana
2) ni sehem moja wapo lakini sio kigezo kwamba ukianguka smama tena utafanikiwa, izi mythms znatengenezwa na media kuuza story ila wapo wngi sna waliojaribu na walikufa maskini
3) as long ni biashara basi kuna sehem ishatengeneza matajiri mpaka ikajulikana
4) izi ni falsafa za media, utajiri hauji kwa sababu ya juhudi ila kuna namna tu dunia inaamua nan apate nan akose unless uibe ama uzaliwe wa kishua

5) maelezo ya media yale yale, watu wengi wanafanya kazi kwa bidii na hawatoki unaowaskia wewe ni wale waliofanikiwa tayar ila wapo wengine nyuma story zao ziliishia kimskini
 
Back
Top Bottom