Kulingana na namna malalamiko yamekuwa mengi sana kwenye suala la namna ya kutuma maombi ya ajira za serikali kupitia mfumo uliopo kwa sasa ambao maombi yote hupitiwa na binadamu ambao uzoefu unaonesha kuwa huwa na maslahi ya binafsi ya wazi ama kificho kwenye kuchagua waombaji wapi wapatiwe ajira.
Masuala kama ukabila yamejadiliwa sana,nakumbuka kipindi cha mwendazake zilizushwa tuhuma kuwa watu wa kabila la wasukuma wanapatiwa kamserereko fulani kwenye upande wa ajira serikalini.
Pia watoto wa viongozi imekuwa ikilalamikiwa kuwa nao wanasaidiwa kupata ajira serikalini,bila kusahau wazee wa mikono mirefu nao wamekuwa wakituhumiwa kutumia vijipesa vyao kuwawezesha wapendwa wao kupata nafasi za kazi serikalini
Sasa kwa sababu ya udhaifu huu wa binadamu kuwapatia upendeleo baadhi ya watuma maombi naona imefika wakati sasa itumike teknolojia ya blockchain yenye mfumo wa smart contract kuprocess maombi yote ya waombaji kulingana na vigezo vitakavyowekwa na muajiri.
Hii teknolojia sio ngumu sana kuiplement kwani itahitajika mafunzo ya muda mfupi tu ya wataalam wa IT wa TAMISEMI kuweza kuitengeneza na inaweza ikawa ndio muarobaini wa ajira za serikali kutolewa kiupendeleo.