Huu ndio wakati sahihi wa kurekebisha game yetu ya Bongo Flavour

Huu ndio wakati sahihi wa kurekebisha game yetu ya Bongo Flavour

Joined
Oct 16, 2020
Posts
92
Reaction score
196
Asalaam alaikum ndugu zangu, habarini za usiku. Kwanza poleni na majukumu yenu ya siku nzima na Mungu awape nguvu na afya za kuwawezesha muamke mkiwa fit katika majukum yenu ya kujenga Taifa.

Kuna msemo unasema "ACHA INYESHE TUONE PANAPO VUJA"Kinacho endelea mitandaoni hizi siku mbili nakichukulia kama mvua inayo nyesha ili tuone panapo vuja.

Baada ya sakata la baadhi ya wanaojiita wanaharakati kumpinga kijana mpambanaj anae itangaza nchi, eti kisa yeye ni mwanachama wa CCM, mara ataitumia tunzo kama fimbo ya kuwachapia wapinzani wake. Inachekesha lakin hii ndio Tanzania kila kitu kinawezekana hapa.

Kitu kilichonifurahisha ni kua baada ya wanaharakati wale kuona kama wameshinda ile vita siku ya jana ni hii reaction ya leo. Baada ya wasanii, watangazaji, waigizani, bloggers, businessmen, wadau na wapenzi wa muziki wote kumsapoti Diamond na kusambaza upendo hata wale walio onekana walikua wanatofauti tangu zamani.

Diamond hata asiposhinda hii tunzo lakini sisi kama nchi tumesha shinda, maana tumepiga hatua moja kubwa ya kutoa matabaka yote na chuki iliokua inakithiri katika tasnia ya burudani.

Huu ndio muda sasa wa kurudi na kuanza kusupot hustling za vijana wenzetu katika kila angle bila kujali matabaka.

Ikitokea tuzo amekua nominated msanii wetu yeyote tuibebe kama nchi na tuisapoti na hapo tutakua tumepiga hatua kubwa mno.

NB:LOVE ALWAYS WIN OVER HATE
 
Wanaharakati huwaga wana hubiri uhuru "uhuru wa kuchagua........mara sijui uhuru wa vyombo vya habari........uhuru wa maoni.........",ila diamond ametumia uhuru huo huo wa kuchagua chama anacho kiamini ishakuwa nongwa.

Sasa unajiuliza labda wana definition nyingine ya UHURU.
 
Asalaam alaikum ndugu zangu,habarini za usiku.Kwanza polen na majukumu yenu ya siku nzima na Mungu awape nguvu na afya za kuwawezesha muamke mkiwa fit katika majukum yenu ya kujenga Taifa.
Usichokijua hata hao celebrity, blogger's wanaompost hawataki ashinde Ni unafiki tu umetawala kijana anashombo sana mwambieni apunguze maneno na ujuaji.
 
Acha upumbavu, mnaanzisha chuki lakini hamtaki ziwarudie. Mimi ni shabiki wa domo lakini siwezi kumsapoti katika hili,nitaendelea kudownload nyimbo bure na kuburn,sitakuja kununua kazi yake maana mafanikio yake yanampa kiburi anajiunga na wanaotesa watanzania wenzake.
 
Diamond anahitaji sapoti sababu anawakilisha Tanzania
Ila Naseeb asingepitishwa katika hili analolipitia saivi baada ya kushinda hio tuzo nadhani hata wewe unajua kejeli na dharau angezozitoa

'Waite wasanii wako wote bongo wapige show na mimi npige peke angu ntajaza' Diamond platnumz
 
Asalaam alaikum ndugu zangu,habarini za usiku.Kwanza polen na majukumu yenu ya siku nzima na Mungu awape nguvu na afya za kuwawezesha muamke mkiwa fit katika majukum yenu ya kujenga Taifa.
Mmerudisha mpira kwa kipa .. Acheni ujinga .. Kamati ya kupiga kura si ni watu 500 tu mnaumia nini... Ndio mtajua kuna kende za mfungo na kende za kutia mimba ...mtulieeee
 
Yaani maisha hayo ni sawa na maisha ya Samaki baharini,

Samaki baharini wanakulana wao kwa wao!
 
Acha upumbavu,mnaanzisha chuki lakini hamtaki ziwarudie.
Mimi ni shabiki wa domo lakini siwezi kumsapoti katika hili,nitaendelea kudownload nyimbo bure na kuburn,sitakuja kununua kazi yake maana mafanikio yake yanampa kiburi anajiunga na wanaotesa watanzania wenzake.
Ulitaka wote tuwe wapinzani kaka...?
Siasa hazipo hvyo,we penda chadema me ntaipende ccm, hata shetani ni mbaya ila anawafuasi wake pengine na ww n mmoja wapokwa sababu mtu wa mungu hawezi kuwa na chuki kwa binadamu mwenzake pasipo sababu
 
Diamond anahitaji sapoti sababu anawakilisha Tanzania
Ila naseeb asingepitishwa katika hili analolipitia saivi baada ya kushinda hio tuzo nadhani hata wewe unajua kejeli na dharau angezozitoa

'Waite wasanii wako wote bongo wapige show na mimi npige peke angu ntajaza' Diamond platnumz
Hivi hua unasoma tweet za burnaboy.Au hua unaangalia awards show,watu wanatoa shades mno.Lets say leo kiba anamuita Sadala ulitaka diamond ashinde tuzo alaf asiseme chochote are u serious.Hayo ndio maisha y music industry bro
 
Ulitaka wote tuwe wapinzani kaka...?
Siasa hazipo hvyo,we penda chadema me ntaipende ccm, hata shetani ni mbaya ila anawafuasi wake pengine na ww n mmoja wapokwa sababu mtu wa mungu hawezi kuwa na chuki kwa binadamu mwenzake pasipo sababu
Nani kakaako wewe?
Mimi ni mfuasi wa shetani ndiyo.
Lakinj MwanaCCM yoyote ndiye shetani mwenyewe.
 
Back
Top Bottom