DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Tukubaliane kwamba CHADEMA kuingia madarakani ni kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Ni Jambo ambalo litahitaji maandalizi ya muda mrefu na tofauti na wengi wanavyo fikiria kutokuwa na tume huru au katiba mpya sio sababu inayowakinga.
Tofauti na kipindi cha awali, serikali ya awamu ya tano na sita imefanya mageuzi makubwa kwenye kufanya kampeni kali ambayo imesababisha Rais Samia na Magufuli kipindi alipokuwa hai kuwa maarufu sana. Mafanikio ndiyo yapo, ila yamekuzwa na vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuwapa wananchi hamasa kubwa. Imefika hatua ambayo serikali imelipia matangazo ya Instagram na ya barabarani ili kutangaza mafanikio ya Rais Samia. Lakini mafanikio yapo kweli, pia ni kweli kwamba wananchi wanaikubali sana serikali ya Rais Samia Kwa kiasi kikubwa kuliko sera na harakati za wana CHADEMA…
Nini sasa kiwe kipaumbele Kwa walio CHADEMA?. Inabidi tuangalie motisha ya yeyote kuingia kwenye siasa au kuwa mwanaharakati. Wana CHADEMA wanaendelea kupitia ugumu katika harakati zao za kupigania haki nchini. Hawatakiwi kukatishwa tamaa kwa kutokushinda uchaguzi kwasababu harakati za kweli zinatoka moyoni. Wanatakiwa kuamini kwamba siku moja kazi yao itazaa matunda katika mchakato wa kuwa na Tanzania mpya. Wanatakiwa wachukulie yanayo wakuta positively wakilenga kuhakikisha kwamba haya mtokei mwingine hata katika vizazi vijavyo. Huu ndio wito, hiyo ndiyo kazi nzito…
Mabadiliko huchukua muda, kukaa meza moja inahitaji juhudi kali, ila kwa kuzingatia niliyo yaeleza, utagundua kwamba hiyo ndiyo attitude inayofaa. Huo ndio uzalendo wa kweli…..