Huu ni mkakati maalumu wa kupata pesa

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Jaribu kufanya hivi hata mwezi mmoja tu uone utapata sh. ngapi?

Moja ya siri ya mafanikio ni pamoja na ubahili, ufuatao ni mkakati ambao utakufanya uwe moja kati ya mabahili wakubwa ndani ya mwezi mmoja baada ya kuona matokeo yake utachagua kuendelea kuwa bahili au uache ubahili.

1. Kama kila siku ukitoka kazini huwa unapitia kunywa bia, piga hesabu huwa unakunywa bia ngapi kwa siku. Kama ni bia 3 za sh. 2000, maana yake ni kwamba unatumia sh. 6000, basi mwezi huu usinywe bia kisha kila siku uwe unapitia Mpesa unaweka sh. 6000 ili kuweka pesa yako.

2. Hakikisha kila unapojisikia kunywa supu asubuhi ambayo ni sh. 3000 mpaka sh. 5000, basi kunywa chai na chapati zako kiasi kinachobaki kaweke Mpesa.

3. Wale ambao huwa wakikuomba hela hata kama hauna huwa unahakikisha unatafuta mpaka unawapa, mwezi huu kama amekuomba laki moja mwambie sina kisha nenda Mpesa kaweke hiyo laki moja.

4. Wale wa michango ya harusi, vipaimara n.k wakija kukuomba mchango usitoe waambie sina, kisha ile pesa waliyoomba uwape mchango nenda kaweke Mpesa. Ila misiba changia tafadhali kwani ile ni dharura na si starehe.

5. Kama wewe ni mtu ambaye kila ukiona nguo nzuri lazima ununue, siku ukivutiwa na nguo ambayo unahisi kwa akili zako ni lazima ununue, jizuie usinunue kisha ile bei yake nenda kaweke Mpesa.

6. Kama wewe ni mtu wa kununua vocha pasipo na matumizi ya msingi bali kuchat tu, hakikisha unanunua vocha panapokuwa na sababu ya msingi tu, kiwango cha pesa kinachobakia katika ile bajeti ya siku za nyuma kaweke Mpesa.

7. Kama wewe ni mtu usiye na gari lakini huwa unapanda bajaji au bodaboda bila sababu ya msingi na unapoenda si mbali, mwezi huu acha hiyo pesa kaweke Mpesa.

8. Kama wewe ni mtu wa kwenda Beach kila weekend, kiingilio kuanzia elfu sita na kuendelea na vinywaji ni gharama. Mwezi
huu usiende kisha pesa yote kaweke Mpesa

9. Kama wewe ni mwanaume, unafahamu fika ukiweka appointment na mpenzi wako au ukitoka out na mke wako huwa unatumia pesa nyingi, mwezi huu mke wako au mpenzi wao akikuomba mtoke out mwambie nimetingwa na kazi, baada ya hapo kaweke hela yako Mpesa.

10. Sitisha offer yoyote ile isiyo na ulazima, iwe bar, restaurant, kwenye daladala au popote pale.

IKIFIKA MWISHO WA MWEZI ANGALIA ACCOUNT YAKO YA MPESA INA SH. NGAPI KISHA UTACHAGUA KUENDELEA NA HUO
MFUMO AU KUACHA.

NB: Nimependekeza mobile banking kwani itakusaidia kuepukana na foleni za bank, pia hautaona aibu kwenda kuweka hata elfu mbili Mpesa tofauti na bank. Karibu kwa maboresho ya wazo hili.

Asanteni sana.
Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

AT YOUR OWN RISK
 
Wewe ni stakeholder wa VODACOM?kwanini wasiweke tigopesa
 
Ahsante sana Ushauri mzuri hasa kwa wanaopata kipato cha juu kuanzia laki nne kwenda jui jaribu kufikiri kwa mtu anapata net salary ya 364,000/-
hanywi pombe., si muhongaji wa hela..
ni mvulana anajipikia
anategemewa na wadogo zake watatu wapo sekondari wawili ni private school
Kuna hela ya nauli kwenda kazini
Fungu la kumi ,zaka na sadaka.
Hela ya Umeme na maji karibu 30,000 kwa mwezi..
Chakula siri gengeni sawa..

Hebu hapo msaada kidogo ndugi yangu mchunguzi huru
 
me mbona godoro ninalo siwezi kulalia mapesa wakati mapesa yanatafutwa ili yatumike..km ndo hvyo uchumi hautakuwa maana bar/machinga/mitandao nk cwatalala njaa...
 
me mbona godoro ninalo siwezi kulalia mapesa wakati mapesa yanatafutwa ili yatumike..km ndo hvyo uchumi hautakuwa maana bar/machinga/mitandao nk cwatalala njaa...

kwani pesa ukiweka bank ama mpesa si iko kwenye mzunguko tayari
 

Hakuna solution ya matatizo ambayo inaweza kutatua matatizo yanayowakumba watu wote, lakini nilichowasilisha hapo juu kina uwezo wa kuwasaidia watu weng sana. Kwa kesi yako mimi nawewe tufikiri mbadala wa hilo.
ASANTE
MCHUNGUZI HURU
 
Last edited by a moderator:
me mbona godoro ninalo siwezi kulalia mapesa wakati mapesa yanatafutwa ili yatumike..km ndo hvyo uchumi hautakuwa maana bar/machinga/mitandao nk cwatalala njaa...

Nawewe kuna siku utakuja kuwa baba au mama wa familia??? Aiseee
 
Michango ya harusi huwa na lawama sana aisee.
Bora mizinga ni rahisi kuipotezea.
 
umetisha kaka mawazo mazuri

NB: mtz huru picha yako inatisha jameni
 
Michango ya harusi huwa na lawama sana aisee.
Bora mizinga ni rahisi kuipotezea.

Daah!! Acha kabisa kaka, nina kadi kama nane hapa na zote ni watu wangu!! Kadi ya gharama ya chini kabisa ni 40,000/ can you imagine maisha yanavyofanywa kuwa magumu jamani!
 
Daah!! Acha kabisa kaka, nina kadi kama nane hapa na zote ni watu wangu!! Kadi ya gharama ya chini kabisa ni 40,000/ can you imagine maisha yanavyofanywa kuwa magumu jamani!
halafu siku hizi wanaweka na viwango vya kutoa kabisa. sometimes ni bora kujitoa ufahamu liwalo na liwe tuu vinginevyo utajikuta huendelei.
 
kwa mara ya kwanza nimeona uchunguzi wako ukiwa na mantiki
 
Inawezekana kufanya mengi ya hayo, ila suala la kumpa hela mtu muhitaji hilo siliwezi kabisa. Yani i have it in me, nimeshindwa kabisa kuacha suala la kumpa mtu pesa hata kama najiumiza mimi, sometimes nahisi labda nipo hivyo ili wengine waishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…