Huu ni mmea gani?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nimeukuta mkoani Kigoma. Wenyeji wanasema matunda yake ni matamu na yanaliwa.

Huenda ni dragon fruits ya Kiafrika?

Inasemekana, dragon fruits ni kati ya matunda ghali sana Afrika Mashariki! Ninataka nikaipande shambani kwangu.

Kuna mtu anayefahamu kama yana soko?

Kama yana soko, nitaipanda mingi.

 
Nimeshawahi kula sana enzi za utoto Njombe. Bahati mbaya jina lake kwa kiswahili sijui hata kingereza pia.
 
Umeshindwa hata ku gugo mkuu...hiv hik kizaz mbona kina vilaza sana aisee...yaan ni kizaz cha kutafuniwa kila kitu..dah
 
Sisi wakati tunakua tulikuwa tunauita washawasha
 
Waha wanaiita NTARE au MKONO WA SIMBA
 

Attachments

  • IMG_20231217_150049_438.jpg
    956.6 KB · Views: 1
  • IMG_20231217_145429_899.jpg
    1.2 MB · Views: 2
Nimeshawahi kula sana enzi za utoto Njombe. Bahati mbaya jina lake kwa kiswahili sijui hata kingereza pia.
Njombe! Kumbe yanastawi hata maeneo ya baridi! Nilifikiri ni mimea ya ukanda wa "semi arid"
 
Nimeshawahi kula sana enzi za utoto Njombe. Bahati mbaya jina lake kwa kiswahili sijui hata kingereza pia.
Ni kweli yapo mengi sana ukanda wa Makambako, Wanging'ombe, Ilembula, Mtwango, Saja
 
Hayo cactus ndio huyajui?
Kweli watu hamna hata exposure ya ndani ya nchi?
Nenda Kawe pale karibia na Shule ya Feza yamejaa kibao.
 
Chakula safi sana hiyo ya Wachunga Ng'ombe porini. Ingawa inapaswa ulipasue kwa ustadi maana lina tumiba tudogo tudogo juu ya ganda, ukijichanganya ulimi udungwe kazi unayo.
Pia ukila hilo tunda ni kama pera, mbegu zake mzee zitarejea zimekodoa kodooo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…