Huu ni mmea gani?

NJoo Dodoma yapo bure!
 
Ila watu tunatofautiana! Watoto wa mjini tunawafungia ndani kama kuku! Nahisi hata watoto wangu watakuwa hawaujui huu mti. Jamani ambao bado mna wazazi hakikisheni watoto wenu wanaenda kusalimia babu na bibi zao wakachunge na ng'ombe! Mkubwa mzima hajui Cactus (Opuntia spp). Enzi zetu tumekula sana matunda yake machungani!
 
Mkuu niliona ya na demand kubwa ila kupitia kwenye mtandao na vipindi vya TV. Fanya research mzee si unajua yale ya sungura wana soko halafu wafuge uone sasa
🤣🤣🤣

Nashukuru mkuu🙏
 
Sidhani kama kuna mkoa Tanzania hii hakuna miti hiyo.
Nimeyala Iringa, nimeyaona Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida, yapo pale kwa Mwamposa Feza Kawe.
🙏🙏🙏
 
Hapana na sijawahi ona yakiuzwa,mara nyingi mti huu hujiotea hasa maeneo ya ukame. Matunda yake ni matamu
Lakini dragon fruits nayo hustawi zaidi maeneo yenye asili ya ukame. Kwa mara ya kwanza nimelila mwaka huu. Ni tunda moja lenye ladha nzuri sana, tamu!

Ila kuna members yanapatikana Iringa na Njombe pia, maeneo ambayo kimsingi ni maeneo ya baridi.

Tuseme ni matunda yanayostahimili hali yoyote ya hewa?
 
Itakuwa ni jamii yake ila sidhani kama una soko , ni kweli matunda yake yanaliwa ila ukila mara ya kwanza unaweza usione uzuri wake(ladha) ni kama matunda pori


Unapatikana hasa maeneo ya ukame kama singida ,Dodoma nafikiri kugoma pia kuja hali hewa inayofanana na hiyo
 
Yote hayo ni maeneo ya semi arid.

Semi arid regions: DODOMA, SINGIDA, ARUSHA, MARA, KIGOMA, MWANZA, SHINYANGA, etc.
 
Mafurahisha hayo au kwa kizungu ni cactus plant
Nilikuwa najaribu kuvuta picha ila ulipotaja jina mafurahisha umenikumbusha mbali hili jina lilitumika kitambo sana somewhere tukiwa watoto.Na Kwa majina ya asili au Kiswahili nadhani inategemea na eneo husika.Kama hilo jina mafurahisha siyo linatumika maeneo yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…