Huu ni msimu wa uuzaji mahindi na wanunuzi wakuu ni serikali, lakini nimetembela maghala kadhaa hakuna mashine ya kupepeta

Huu ni msimu wa uuzaji mahindi na wanunuzi wakuu ni serikali, lakini nimetembela maghala kadhaa hakuna mashine ya kupepeta

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Huu ni msimu wa uuzaji mahindi na wanunuzi wakuu ni serikali, lakini ajabu nimetembela magodawni kadhaa hakuna mashine ya kupepeta taka kama hii hapa chini.

Wanatumia sefa za waya ambazo kwa kutwa sefa moja haimalizi tani30 lakini hiyo mashine inarahisisha kazi kwa kutwa inamaliza tani90. Serikali fanyeni hima mnunuwe hii kwenye magodawni yote.

Pia kuna mashine za kuchambuwa vipande vya magunzi, mahindi yaliyooza hata yaliyokatika mnunuwe hizi itasaidia mahindi yakiletwa kwenu mnasafisha chap mkulima mnamkata gharama za usafishaji.

Pia zipo mashine za kukausha mahindi hii inasaidia mtu anavuna mahindi hata kama hayajakauka vema yanakaushwa kwa mashine na mkulima anawahi kulima tena ktk msimu mmoja.

IMG_20240801_222607_1.jpg
 
Hii mashine ya kusafisha ni bei gani?
Na mashine ya kukausha ni bei gani?

Je sido hawatengenezi? Je ni bei gani?
 
Serikali ya CCM imekusikia..ila ngoja wamalizane na ngedere wakata umeme Kwenye tren watakurudia nawe na wazo lako hiliii ,,ipe mudaa..
Ila Serikali hii imegeuka kituko kwa wananchi aisee.ila inapenda sifa kuliko.
 
Huu ni msimu wa uuzaji mahindi na wanunuzi wakuu ni serikali,lakini ajabu nimetembela magodawni kadhaa hakuna mashine ya kupepeta taka kama hii hapa chini.Wanatumia sefa za waya ambazo kwa kutwa sefa moja haimalizi tani30.lakini hiyo mashine inarahisisha kazi kwa kutwa inamaliza tani90.Serikali fanyeni hima mnunuwe hii kwenye magodawni yote.Pia kuna mashine za kuchambuwa vipande vya magunzi,mahindi yaliyooza hata yaliyokatika mnunuwe hizi itasaidia mahindi yakiletwa kwenu mnasafisha chap mkulima mnamkata gharama za usafishaji.Pia zipo mashine za kukausha mahindi hii inasaidia mtu anavuna mahindi hata kama hayajakauka vema yanakaushwa kwa mashine na mkulima anawahi kulima tena ktk msimu mmoja.View attachment 3058552
Kazi ya sekta binafsi ni ipi?
 
Maghala ni gear ya 2025
Wakulima wenye uelewa wamehifadhi mahindi majumbani.

Kulima alime mkulima then mpanga bei na muuzaji ni serikali HOW N WHY?????

Serikali isiyosikia

WaKenya wananufaika sana na jasho la wakulima wa Tz bara.
Ni lini serikali itachukua maamuzi ya kukuza uchumi wa Tz kuliko wanachofanya sasa.

Maparachichi Mbao mahindi vitunguu matunda mafuta ya alizeti avacado karanga etc WaKenya wanasafirisha nje huku wameweka label Product of Kenya… Wakenya wanalima wapi?

Wakuu wa mikoa mnaififisha juhudi za wakulima. Njombe Mbeya Ruvuma inawahusu

Rushwa inalitafuna Taifa kuliko siku za sodoma na gomora.
 
Back
Top Bottom