Majukwa mengi ya JF kwa sasa hufanya vizuri sana kwenye SEO za google hasa kwa lugha ya Kiswahili.
Nawashauri muunde 'Content Marketing Team' itakayokuwa na kazi moja ya kutafuta wadhamini wa thread mbalimbali zinazoshushwa hapa JF na wanaJF. Namaanisha zile thread za kuelimisha ama kuelezea chochote chenye mantiki kwenye jamii.
Inakuwa hivi kwa mfano:
Thread za
Mshana Jr zinazohusu masuala ya uchawi zinadhaminiwa na wale jamaa wanaojihusisha na uchawi.
Thread za
barafu zingekuwa zinadhaminiwa na mashirika ya ndege ama wakala wa kukata tiketi za ndege.
Thread za
mRick zinazohusu masuala ya biashara zinadhaminiwa na business consultants, makampuni, n.k.
Tunaomba JF kupitia kwa @maxence mello sisi wanaJF tunaoshusha thread zenye maana tuanze kuingiza kipato. Hicho kipato wanashare JF na mwenye thread.
Ni rahisi sana:
JF waanze kuunda jukwaa maalum linaitwa 'JF Content Marketing'. Jukwaa hilo huwezi kuwa mchangiaji wa hovyo hovyo tu ili usije ukaharibu 'business brand' ya watu. Kuanza unaomba uwe member wa hilo jukwaa yaani uweze kuchangia (japo jukwaa unaweza kusoma hata ukiwa guest). Then, jukwaa linafuatilia kwa ukaribu zaidi zaidi zaidi kuliko hata majukwaa mengine.
NB: Naomba mnishirikishe kwenye strategies za namna ya kuingiza hiki kipato. Huu ni muda wa kuangiza pesa kupitia 'visitors' na 'content marketing'
Naomba kuwasilisha.