KERO Huu ni Mwaka wa pili sasa hatujapata vyeti vya kuhitimu Chuo cha Kilimo cha Igabiro (Kagera), kila tukienda wanatuzungusha

KERO Huu ni Mwaka wa pili sasa hatujapata vyeti vya kuhitimu Chuo cha Kilimo cha Igabiro (Kagera), kila tukienda wanatuzungusha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
Mimi ni Mkazi wa Mkoa wa Kagera Wilayani Muleba ni muhitimu wa Diploma in Animal Health and Production katika Chuo cha Igabiro Training Institute of Agriculture kilichopo Muleba.

Tangu tulipohitimu, huu unaenda Mwaka wa pili sasa, tulihitimu Februari 2023 lakini mpaka leo hatujapata vyeti vyetu, kila tukifatilia chuoni jibu tunalopewa ni vyeti bado.

Tukifatilia wizarani tunaambiwa vyeti hutolewa chuoni, kiukweli tumechoka hatuoni jitihada zozote wala ushirikiano wowote kati ya Chuo, Wizara na sisi wahitimu.

Tunakosa fursa nyingi kwa kuwa hatuna vyeti na umri nao unasogea kwa kuwa kuna baadhi ya fursa zinaendana na kigezo cha umri.

Baada ya sisi kuna wenzetu wengine waliohitimu Septemba 2023 nao kama sisi hawajapata pia vyeti, tunajiuliza inakuwaje vyeti vinachukua miaka miwili wakati Vyuo vya binafsi vinasifika kwa kuwajibika mapema na haraka.

Pia soma
~
Chuo cha Kilimo cha Igabiro (Kagera) chakiri Wahitimu hawajapata vyeti kwa miaka miwili, chasema ni suala linalohusu mamlaka za Serikali
~ Huu ni Mwaka wa pili sasa hatujapata vyeti vya kuhitimu Chuo cha Kilimo cha Igabiro (Kagera), kila tukienda wanatuzungusha
 
Back
Top Bottom