kabila01
JF-Expert Member
- Apr 21, 2009
- 4,235
- 4,964
habari wana Jamiiforums
nimejitokeza niweze kupata mawazo na kueleweshwa kutoka kwa ndugu zangu wana Jamii.
Kuna shirika moja lilitangaza nafasi za kazi ya Uhasibu na wakasema sifa za muombaji awe na shahada ya Uhasibu au utawala na Biashara.
Kilichoniacha hoi ni pale tulipoitwa kwenye Interview kati ya watu 30 tulioitwa tuliosomea uhasibu pamoja na utawala wa biashara tulikua jumla wanne tu na post zilikua saba. wengine walikua wamesoma kilimo, Sheria na uchumi. cha kushangaza ni kwamba waliopita kwenye ile interview ni wale waliosoma kilimo na sisi wote tuliosoma Uhasibu, Uchumi na Biashara tukapigwa chini.
sasa hapo nashindwa kuelewa kwamba kwa sababu waliosoma kilimo ndani yake eti walisoma somo la uhasibu ndo wakapata nafasi na sisi tuliosoma Uhasibu kwa miaka mitatu pamoja na mazoezi ya vitendo ya uhasibu tukapigwa chini ni kwamba tulishindwa kujieleza kwenye usail au ndo Ufisadi ndani ya ajira.
Naomba mnisaidie wana jamii kunielewesha hapo