Huu ni ugonjwa gani wa vifaranga vya kuku?

Huu ni ugonjwa gani wa vifaranga vya kuku?

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Wanajf ninaomba msaada kuhusu ugonjwa huu wa vifaranga vya kuku! Kwenye sehemu ya haja kubwa anatoa kinyesi laini mithili ya mapovu! Mwishowe mapovu hayo hukauka na kuwa magumu mwishowe vifaranga hudondoka na kuiaga dunia!

Mwenye uelewa anisaidie, huo ni ugonjwa gani, unatibiwaje! MSAADA WA HARAKA PLEASE MAANA VIFARANGA VINAISHA!

MAELEZO MENGINE YAPO KWENYE PICHA HAPA CHINI👇

IMG_20230302_085026.jpg
UGONJWA WA VIFARANGA.jpg
 
Pole sana,

Huo ugonjwa unaitwa Pullorum Disease (PD)/Salmonella Disease (SD) mara nyingi huwakuta vifaranga.
Dalili zake ni kama ulizotaja

Dawa yake ni Esb3 au Vitacox pamoja na vitamins uwape kulingana na maelekezo ya dawa husika.

Kwa kuwa tayari wameanza kufa cha kufanya chukua maji ya uvuguvugu na kitambaa laini, chovya kisha uwapanguse matakoni hapo kinyesi kilipoziba ili kuruhusu kinyesi cha tumboni kutoka la sivyo watakufa wengi zaidi. Wanakufa kwa sababu wanakula lakini sehemu ya haja kubwa imeziba so wanashindwa kunya.

Zaidi ya yote zingatia sana usafi wa banda, vyombo vya maji na chakula pamoja na maji unayowapa ili kuzuia maambukizi mapya ya vimelea vya magonjwa mengine.
 
Wanajf ninaomba msaada kuhusu ugonjwa huu wa vifaranga vya kuku!Kwenye sehemu ya haja kubwa anatoa kinyesi laini mithili ya mapovu!Mwishowe mapovu hayo hukauka na kuwa magumu mwishowe vifaranga hudondoka na kuiaga dunia!Mwenye uelewa anisaidie,huo ni ugonjwa gani,unatibiwaje!MSAADA WA HARAKA PLEASE MAANA VIFARANGA VINAISHA!MAELEZO MENGINE YAPO KWENYE PICHA HAPA CHINI👇
Wapigie hawa Farmers Centre watakusaidia. Ni madaktari wa mifugo wazuri:
0778 300 300 au 0677205070
 
Pole sana,
Huo ugonjwa unaitwa Pullorum Disease (PD)/Salmonella Disease (SD) mara nyingi huwakuta vifaranga.
Dalili zake ni kama ulizotaja
Dawa yake ni Esb3 au Vitacox pamoja na vitamins uwape kulingana na maelekezo ya dawa husika.

Kwa kuwa tayari wameanza kufa cha kufanya chukua maji ya uvuguvugu na kitambaa laini, chovya kisha uwapanguse matakoni hapo kinyesi kilipoziba ili kuruhusu kinyesi cha tumboni kutoka la sivyo watakufa wengi zaidi. Wanakufa kwa sababu wanakula lakini sehemu ya haja kubwa imeziba so wanashindwa kunya.

Zaidi ya yote zingatia sana usafi wa banda, vyombo vya maji na chakula pamoja na maji unayowapa ili kuzuia maambukizi mapya ya vimelea vya magonjwa mengine.
View attachment 2534442
Nashukuru kwa ushauri! Nitaufanyia kazi pia ninaomba ushauri kuhusu hili pia, kwa kuwa vifaranga hawa wana umri wa siku 3, nilishauriwa niwape Glucose na Neoxchik je, niongezee na hizo dawa ulizonishauri?

Ninamshukuru Mungu dawa ulizonishauri ninazo
 
Back
Top Bottom