Huu ni ugonjwa gani?

Huu ni ugonjwa gani?

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2014
Posts
3,509
Reaction score
3,741
Ugonjwa huu upo sehemu za siri huwa unawasha ukijikuna baada ya muda kidogo unapata naumivu makali, Ngozi ya korodani kuna wakati inakakamaa na kutoa magamba yaani kama nyoka anavyojitoa gamba na yenyewe inakuwa hivyo hivyo.

Nimezunguka hospitality Dawa nyingi nimetumia bila kupona, Dawa nilizotumia zipo za vidongo na za kupaka ambazo ni hizi hapa 1,Cephalexi-250m 2, Alerid, 3, Algic P. 4, Ampiclox. 5, Prednisolone. 6, GentrisoneCream. 7, VClotrimazole Cream. 8, Gentalane Cream , 9, Dermaquat Cream, 10. Candistat. 11. Terbifin-25 12,Flucan, 13 na Grencet.

Dawa zote hizo nimetumia lakini bado, Huu ni mwezi wa nne tatizo lianze, Madaktari wa ngozi tofauti tofauti nimewaona ndo walikuwa wakiniandikia hizo Dawa, Sasa mwenye kujua huu ugonjwa na tiba Yake anielekeze, Ahsanteni
 
Muone dermatologist ufanyiwe skin test ikiwezekana wana Julia kipande kidogo cha ngozi kinapelekwa lab.

Inaweza kuwa aggressive fungal infection ambayo inahitaji kutobiwa kwa dawa za kunywa zizunguke kwenye damu.
 
Muons dermatologist ufanyiwe skin test ikiwezekana wana Julia kipande kidogo cha ngozi kinapelekwa lab.

Inaweza kuwa aggressive fungal infection ambayo inahitaji kutobiwa kwa dawa za kunywa zizunguke kwenye damu.
 
Mkuu serious kabisa,nakushauri...ukaoge kwenye bahari,nimeongea nilichoshuhudia,fanya kama mara mbili,trust me it works
 
M
Ugonjwa huu upo sehemu za siri , huwa unawasha ukijikuna baada ya muda kidogo unapata naumivu makali, Ngozi ya korodani kuna wakati inakakamaa NA kutoa magamba yaani kama nyoka anavyojitoa gamba NA yenyewe inakuwa hivyo hivyo ,Nimezunguka hospitality Dawa nyingi nimetumia bila kupona, Dawa nilizotumia zipo za vidongo NA za kupaka ambazo ni hizi hapa 1,Cephalexi-250m 2, Alerid, 3, Algic P. 4, Ampiclox. 5, Prednisolone. 6, GentrisoneCream. 7, VClotrimazole Cream. 8, Gentalane Cream , 9, Dermaquat Cream, 10. Candistat. 11. Terbifin-25 12,Flucan, 13 na Grencet. DAWA ZOTE HIZO NIMETUMIA LAKINI BADO, Huu ni mwezi wa NNE tatizo lianze, Madaktari wa ngozi tofauti tofauti nimewaona ndo walikuwa wakiniandikia hizo Dawa, Sasa mwenye kujua huu ugonjwa NA tiba Yake anielekeze, Ahsanteni
mkuu nunua mafuta ya dill pakaa
 
Tumia ZOA zoa

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Turudi nyuma kwanza, unatumiaga sabuni gani kwakuoga. Kwasababu miaka ya nyuma nilikuwa najikuna na ngozi ya korodani ilikuwa inakakamaa hivo hivo na kutoa magamba. Kumbe tatizo ilikuwa mi mwenyewe nilikuwa naipenda sabuni zenye detol kwakuogea na nikimaliza kuoga naipaka kwenye ngozi ya korodani. Baadae iliniletea muwasho wa ajabu na ngozi kubabuka ilinigarim sana kugundua hilo tatizo ambalo hata madaktari hawatambui shida iko wapi. Niligundua mwenyewe baada ya kuacha hiyo sabuni kwa cku mbili nikaona na muwasho nao ukipungua.

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni Pumb..u erosion
Dawa yake white field ya maji ya rangi ya kijani ukipaka jifumgie chumbani washa feni speed ya mwisho elekezea huko.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Hilo tatzo litakua kwenye mzunguko wa damu kwa kua limekua la kujirudiarudia tayar limekua sugu..hivyo basi unatakiwa kwenda hospital wachukue sample ya ya damu au majimaji na waangalie na aina gan ya fungus au bacteria anayeleta shida na wakupe dawa ambayo inatakiwa kuwa ni sindano pamoja na ya kupaka..kwa kpind hiki ukiwa unafanya matibabu jitaid kuacha sehem zako za sir zikiwa kavu yaan futa vzur ukitoka kuoga na ukauke kwan unyevu hujengea mazingira ya kukua tena kwa fungus hata kama utatumia dawa..NB.ustumie tena dawa ukifika mwambie daktar akufanyie culture au kipimo cha dam au au kpimo cha majimaji ya eneo husika..


Sent from my TECNO_N9 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nenda salon yoyote wategeshee wakufanyie sclub na msasa wa mbao kisha wakupake na oli ya engine namba 140 itasaidia hiyo inao nyesha ni msuguano mkali unaopata wakati ku.... Eh!!
 
Hilo tatzo litakua kwenye mzunguko wa damu kwa kua limekua la kujirudiarudia tayar limekua sugu..hivyo basi unatakiwa kwenda hospital wachukue sample ya ya damu au majimaji na waangalie na aina gan ya fungus au bacteria anayeleta shida na wakupe dawa ambayo inatakiwa kuwa ni sindano pamoja na ya kupaka..kwa kpind hiki ukiwa unafanya matibabu jitaid kuacha sehem zako za sir zikiwa kavu yaan futa vzur ukitoka kuoga na ukauke kwan unyevu hujengea mazingira ya kukua tena kwa fungus hata kama utatumia dawa..NB.ustumie tena dawa ukifika mwambie daktar akufanyie culture au kipimo cha dam au au kpimo cha majimaji ya eneo husika..


Sent from my TECNO_N9 using JamiiForums mobile app
Mkuu ubarikiwe sana, Ninashukuru sana
 
pole sana mkuu. kwa maelezo ya haraka hiyo ni fungus. cha msingi nenda hospitali ukapate tiba. Ila ninachokiona pia jitahidi kuzingatia usafi wa mwili na nguo hasa kuvaa nguo za ndani na nje mara moja na kuzifua. ziache zikauke vizuri na piga pasi kabla ya kuzivaa tena. utaona mabadiliko ndani ya wiki tu. Pia jitahidi kuangalia maji unayotumia kuoga kama inawezekana uwe unatumia detol unaweka kwenye maji then unaoga. baada ya muda mfupi utaona mabadiliko.
 
Hao ni fungusi ndio wanafanya hivyo jrb kutumia medicated soap kwa kuoga na pia acha povu likaukie hapo..

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Pole sana, fuata ushauri wa daktari
ikiwezekana pumzika kutumia madawa,
umeyachanganya mno,
vinginevyo angalia na historia ya maisha yako;
pengine umemwacha mke ameamua kukulaani;
 
Inatakiwa uende hospital ukafanyiwe culture & sensitivity ili kujua dawa sahihi ya kutumia.

Ila tatzo lako yawezekana ni Chronic fungal infections, so utahitaji kutumia kwa pamoja dawa ambazo zitaingia direct mpaka kwenye mfumo wa damu (systemic drug) na dawa za kupaka eneo husika (topical drugs)

Pia kupona ugonjwa huo unatakiwa kuna vitu uvifanye zaidi ya kunywa madawa. Ambalo kubwa ni USAFI. Eneo husika hakikisha linakua safi na kavu muda mwingi, nguo zako za ndani uanike juani na sio ndani (au uzipige pasi).

Mda mwingine kuogea masabuni yenye chemicals kali hushambulia mpaka bacteria wa asili wa ngozi (normal flora) hivyo kupunguza ulinzi wa eneo husika.

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom