Salam,
Hapa naona niungane na mchangiaji mada hapo juu, hili suala lako linajibika lakini inakuwa ni vigumu kuweza kukujibu moja kwa moja kwa vile hujajieleza vya kutosha, mfano jinsia yako, umri, mda wa hilo tatizo, unapopata dalili za malaria (unakusudia ukipata homa) siku nyengine jaribu kusherehesha dalili vya kutosha.
Lakini kwenda tu hospitali na kupimwa vipimo vyote ni usumbufu kutokana na mda na gharama, hivyo ushauri kama ni mwanamke ungeona kumuona Daktari wa mambo ya kike inawezekana sana una uambukizo kwenye njia ya uke ua kwenye kizazi, pengine mifupa bali kama ni mwanaume utamuona daktari wa Mifupa.