Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,271
- 2,903
Nimeamua kuandika hili baada ya Kuona kuwa kumekuwa na Upotoshaji Mkubwa kila siku zinavyoenda kwa hizi nadharia mbalimbali za kimatukio wakizihusisha na namba. Conspiracy theories.
Unajimu/utabiri Wa namba ulikuwepo toka zaman sana.miaka na miaka hata kabla ya Kristo. Angalau huko tunazungumzia UTABIRI kama ambavyo nakumbuka miaka ya 90 walikuwepo Watabiri maarufu sana akina Phillip Majura na Dr Matunge kama sikosei.sijui waliishia wapi.
Miala ya nyuma kidogo alikuwepo sheikh Yahya ambaye naye alijulikana kama mtabiri akitumia namba na majini katika tabiri zake ambazo nazo zingine zilitokea na nyingine zilishindwa. Zipo nying tu na alishindwa hata kujitabiria kifo chake kilikuja bila yeye kukiona.
Utabiri wa MAGAZIJUTO huu umekuwa maarufu sana ukihusishwa na Freemason, illuminati,NWO na imani au nadharia mbalimbali. Tusisahau katika hili alikiwepo Nostradamus miaka ming iliyopita na akitabiri mambo mengi ambayo mengine hayakuja kutokea. Nakumbuka hata kifo cha Tupac Shakur kilihusishwa na ile 7 days Theories watu wakiamin baada ya siku/miaka 7 angefufuka au angeonekana.sasa ni miaka nenda rudi ameshaoza huko aliko.
Tukio la 9/11 uchaguzi tayari wadau mbalimbali wameshalifanyia magazijuto ili watimize lengo lao flan. Na hata uchaguzi ungefanyika tar 15/11 zingefanyika hesabu za kujumlisha kuzidisha,kugawanya na kutoa wapate namba ambayo wangeipata.
Swali la kujiuliza tukio la ugaidi la september 11 lilipotokea je mpaka leo haukuwa umefanyika uchaguz? Ulifanyika tarehe gani? Huu wa mwaka huu kufanyika tarehe 9/11 tayari imeshakuwa issue ya kutumia namba kuaminisha watu uongo na kuwachanganya vichwa.
Na haya mambo utaona yanatokea baada ya matokeo yenyewe kutokea si kabla. Nlitaman nimsikie mtu akisema hapo kabla akitumia namba kwa nini trump atashinda na uhusiano wa tereh hiyo na uchaguzi au ushind wa trump. Hakuna aliyefanya hivyo
Dunia sasa inaendeshwa kwa hofu, maigizo,uongo n.k kwa kuamini kila jambo linalotokea kuna watu wana li control hapa duniani. Kitu ambacho si kweli. Ni kuwajengea watu uwezo wa uongo na kuwajengea wengine hofu na woga.
Na hii ndiyo taratibu mpya iliyoanzishwa.kuwajengea watu hofu. Hofu isionekana inaletwa na nani.na ndo maana kuna vikundi vinaitwa secret society, illuminati,freemason,elite society n.k ambao hawa hutumika sana katika kujenga hofu kwa wananchi wasio na uelewa.
Vinaweza kuwepo na sipingani na hilo lakini nguvu zake si yamkini kwa maana zimekuwa ni zakufikirika sana kwa lengo la kuwajengea watu hofu sana. Na kila mwenye mafanikio atahusishwa na makundi moja wapo ya haya awe mwanamichezo,mwanasiasa,mwanamuziki,msanii,mwandishi,mwanadini n.k
Hesabu za kulazimisha matukio yafanane na tunachotaka kuamini ni Hesabu za MAGAZIJUTO zenye lengo la kutufanya wengine tuonekane tulijua jambo hili litatokea n.k
Ni iman mbovu mbovu zisizojenga hata kidogo.