Gashongoile
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 487
- 145
Kwa muda mmrefu sasa kumekuwa na malalamiko mengi kuwa jeshi la Police limekuwa likitumiwa kisiasa na chama tawala,lakini kauli hizo zimekuwa zikipuuzwa. Kutokana na hali hiyo nimepata maswali mengi kichwani kuhusu jambo hilo na baada ya kuwaza kwa muda mrefu nikajikuta nikijiuliza kuhusu matukio mbali mbali ambayo yamekuwa yakifanywa na jeshi la polisi. Bahadhi ya matukio kama ulipuaji wa mabomu kwenye mikutano ya kisiasa hasa ya CHADEMA pamoja na kuwafungulia kesi Makada mbali mbali kila kukicha.
Moja ya matukio yaliyonisikitisha ni hili la juzi ambapo bomu limelipuka tena kwenye Mkutano wa CDM eneo la Mabibo sahara na Polisi bila haibu kuja na majibu mepesi kuwa lililipuka kwa bahati mbaya, arafu mbaya zaidi hawajasema chochote kuhusu waliousika kwenye uzembe huo kama ni kweli ilikuwa bahati mbaya. Hapa swali ni Je hali ingekuwa hivyo kama bomu hilo lingelipuka (Kwa bahati mbaya) kwenye mkutano wa CCM?
Jambo lingine linalozidi kuniakikishia kutumiwa kwa Jeshi ili kisiasa ni ili la kuwafungulia kesi za UGAIDI makada wa CDM. Police hao hao walimfungulia Mkurugenzi wa ulinzi wa CDM kesi ya ugaidi kabla ya ofisi ya DPP kudhalilishwa na Mahakama kuu kwa kuifuta kesi hiyo.
Katika hali ya kushangaza na kuonyesha kuwa katika kesi hizi kuna mkono wa kisiasa ni hii kesi iliyofunguliwa Tabora ya kutuhumiwa kwa Makada wa CDM kummwagia mtu tindikali. yani hii ni Political fubricated case kwa namna yoyote ile. kwanza kosa ni kummwagia mtu tindikali then case inafunguliwa ya UGAIDI. Hivi kweli leo hii mimi nikimmwagia mtu tindikali kwa namna yoyote ile nitafunguliwa kesi ya ugaidi? Na je watuhumiwa wa kummwagia Tindikali Mkurugenzi wa Home Shopping Center nao watafunguliwa kesi ya UGAIDI?
My take:
Madhara ya Kesi hizi(Political fubricated case) katika mfumo wa uendeshaji wa kesi za makosa ya jinai ni mkubwa kuliko mtu wa kawaida anavyoweza kufikiri. Ikiwa kesi hizi zitaachwa kuendelea kufunguliwa inamaana zitatengeneza presidence ambazo madhara yake ni makubwa. Kwa mfano watu wakigombana na mmoja akamwagia Mwenzie Uji wa moto,Maji ya Moto au kitu chochote kikamuunguza uso naye italazimika afunguliwe kesi ya ugaidi. hili ni jambo hatari sana, kumekuwa na matukio ya watu kumwagiwa tindikali, Petrol tena wengine hadi kupoteza maisha lakini sijawahi kusikia mtu yeyote amefunguliwa kesi ya Ugaidi. kuna watu wamewajeruhi watu wengine kwa kutumia silaa za moto kama Bunduki na Bastola Visu Mapanga NK, lakini wanafunguliwa kesi za kushambulia na kujeruhi, au ukitumia Tindikali kumjeruhi mtu ndiyo Ugaidi?
Namalizia kwa kusema tena kuwa kwa matukio haya ni wazi kabisa kuwa Jeshi la Police linafungua kesi hizi kwa msukumo wa kisiasa na kudhiilisha linavyotumiwa na CCM.
Naomba kuwasilisha.