Huu ni utapeli mpya?

Huu ni utapeli mpya?

MtuloBM

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2020
Posts
595
Reaction score
555
Wandugu, Jana katika pita pita zangu huko YouTube nikakutana na hizi habari. Hawa jamaa wanajiita (Mula empire) TANZANIA PAYMENT

wengi ya walionipa Habari za hawa jamaa kupitia YouTube channel zao wanasema ni moja ya njia mpya ya kupata pesa mtandaoni.
Wanasema utaniunga Kwa Tsh 13000/= na utakuwa na kazi ya kutazama video za YouTube na kulipwa kwa kila video.

mambo ni mengi ila kubwa ni kuwa unaweza alika mtu na ukilipwa Tsh 2000.

Kwa anaejua kuhusu hawa jamaa atupatie mwanga🙏🏻

0BB34E2E-ED55-49D1-9A60-C20061F24E87.png
 
Nimeona status za watsup watu wanapenda pesa za dezo daah
 
Wape 15000 yao uwe fursa io 2000 ukilipwa labda jua ligeuze.
 
Kuna vitu vingine sio hata vya kujiuliza unapuuzia tu maana unaona kabisa ni utapeli wa kijinga.

Kwenye hilo tangazo/ maelekezo ya namna ya kulipia kuna ujinga kama vile MUHAMALA,
.............EKA

Watu mna moyo kufuatilia vitu kama hivyo
 
Kama ni kampuni kwanini ulipe kwa mtu binafsi pesa. Duniani ukiamua kutapeli huwezi kosa wa kumtapeli.
 
Kuna vitu vingine sio hata vya kujiuliza unapuuzia tu maana unaona kabisa ni utapeli wa kijinga.
,,,, Kwenye hilo tangazo/ maelekezo ya namna ya kulipia kuna ujinga kama vile .....MUHAMALA,
.............EKA

Watu mna moyo kufuatilia vitu kama hivyo

Tunaelimisha watu mkuu
 
Mkuu acha kutufanya sisi watoto wadogo, hili ni tangazo lako na unahusika nalo
Sina ninachokijua kuhusu Hii mishe. Mm mwenyew ni mgeni. Nigoogle nimeenda YouTube na sehem Zote ninazoweza kusearch. Naomba kufahamishishwa kama Unajua kuhusu hizi Habari
 
Back
Top Bottom