Huu ni wehu wenye povu la omo

Huu ni wehu wenye povu la omo

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Ukitendwa na Mpogoro fulani kwenye Mapenzi
haimaanishi Wapogoro wote ni vimeo, ni mtu
huyohuyo mmoja na matatizo yake..
Ukikutana na Msukuma mwenye Wivu anakufuatilia
hadi harufu ya sabuni unayonukia ukirudi toka kazini
kama ni Ki-eva cha gesti au Imperial uliyoogea asubuhi, haimaanishi Wasukuma wote ni mwabwege
kama huyo jamaa...
Kuna watu wanahukumu watu wengine kwa sababu
tu Jamaa fulani poyoyo la kabila fulani lilimtenda... Ukimtongoza utasikia, ''Ah we Mbena??Ah hapana
aisee, Nimetendwa na Mbena fulani sina hamu na Wabena kabisa''
Ipo Siku utamkataa Mme
uliyeandaliwa kwa sababu tu anafanana kabila na
Msambaa fulani aliyekutenda ukiwa Form 3.. HUO NI
WEHU WENYE POVU LA OMO...
 
kama kawaida mkuu STUNTER anaendelea kutema sumu...

BTW ana mpango wa kuandika kitabu concerning with mapenzi ya kibongo

joke!
 
Back
Top Bottom