Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
1. Kuna watu ambao unakuta muda mwingi anautumia kulalamika X ananichukia, Y ananichukia. Anahangaika kutafuta kupendwa. Why unataka upendwe na kila mtu? UMEKUWA PESA? ukijipenda mwenyewe si inatosha? Mi katika maisha nlijifunza kujipenda mwenyewe. Akitokea na mwingine kunipenda nashukuru na akitokea mwingine kutonipenda nashukuru pia. Ni Wendawazimu kutaka kila mtu akupende.
2. Kuna watu ambao kazi yao ni kutafuta au kuelezea ubaya wa wenzao. X mbaya sana. Ana roho mbaya. Y ni mtu mbaya, ana matatizo haya na haya. Ukiona kila mtu mbaya kwako na kila mtu ana tatizo ujue wewe ndo tatizo. Acha maisha ya kutafuta ubaya wa mtu. Tafuta mema kwa afya yako.
3. Khna wale wenzangu wao kila siku wanaonewa tu...ukiona mtu kila wakati anaonewa ujue ana shida. Ni mlalamishi kama mama alokosa mwana. Hili nalo ni tatizo sana kwa baadhi ya binadamu. Yeye akiguswa bega amegongwa kwa sababu anaonewa. Akikanyagwa kwenye daladala atalalamika siku nzima anaonewa. Ni wendawazimu.
4. Kuna wale ambao wana wazimu wa kutaka kuwa treated special. Yaani anataka yeye awe mahsusi kila sehemu. Atalalamika kwa nini yeye kapewa maji kwenye glass ya bei rahisi wakati wengine wamepewa kwenye glass zenye kiuno. Yeye kapewa kwenye glass imenyooka tu. Anataka kuwa special.
5. Na kuna wale ambao wana wazimu wa kujiona tu wao ni bora kuliko wengine. Wana kosa kujiamini pia. Wanajifichia kwenye vitu hawa ukiwaona hivi na vitu vyao wanaanza kuvielezea. Hii nguo nlinunua 500,000. Hili gari langu ni tofauti na mengine kama hili. Langu lina. Ni wazimu tu kama wazimu mwingine.