Huu si unyanyapaa, nimesaidia rafiki zangu

Huu si unyanyapaa, nimesaidia rafiki zangu

Memtata

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
587
Reaction score
1,863
Habari wadau,
Mimi binafsi nilishawahi kupata kashfa ya UKIMWI, nakumbuka ilikuwa wakati mgumu sana kwangu na niliishi kwa mateso, unyonge na hofu kubwa lakini leo hii kuna mmoja nimesema hadharani habari zake za maambukizi.

Huyu dada niliwahi kuwa na mahusiano naye sasa kwakuwa mzunguko ni huu huu jamaa yangu naye akakutana naye wakati huo mimi nilishaachana naye. Jamaa yangu huyu huwa na mtindo wa kutembea na vipimo vya HIV kabla ya kutembea na huyu binti akaamua kumpima.

Kabla ya kumpima binti alijibaraguza kana kwamba hakuna shida yoyote lakini hii haikumfanya jamaa asitishe zoezi la kumpima, akampima. Mara paap mistari miwili hii hapa kwenye HIV1 na control hii ikimaanisha bint alikuwa na maambukizi. Jamaa akatemana na dem huku akiwa haamini kilichotokea.

Pamoja na kushangazwa na majibu ya bint lakini jamaa akaanza kunifikiria mimi, huyu dem alikuwa wangu kwa muda kabla yake kwahiyo jamaa aliwaza kabisa na mimi inawezekana ni HIV+. Akaamua kunitafuta na kunipa majibu, nilishtuka sana sababu hata mimi si mtu wa kutumia kinga lakini nilijipa moyo sababu hii si mara yangu ya kwanza kunikuta lakini wasiwasi ulikuwepo nisiseme uwongo.

Kilichonichukiza ni kwanini huyu dem hakunijulisha hali yake au alitaka kuniambukiza makusudi!! Nikajikaza nikaamua kabla ya kuanza kumshambulia mtoto wa watu nipime kwanza maana kama na mimi nikikuta ni positive basi sitakiwi kumlaumu sana maana inawezekana mimi ndio nimemuambikiza.

Nikapima bahati nzuri nikakuta sina maambukizi, nilishukuru Mungu kwa hili ila sikuishia hapo nikamtumia huyu dem meseji nikamwambia kwa kifupi tu 'ulikuwa na lengo gani kwangu?' nikaishia hapo. Dem akakaa kimya kwa siku kama tatu hivi kisha akanitafuta kwa kunipigia sikupokea simu. Siku moja nikakutana nae akakataa hata kunisalimia kisha akaondoka na wakati huu alikuwa anaoneoana hayuko normal kabisa kiafya.

Ili kuwaokoa rafiki zangu wa karibu nikaamua kuliweka jambo hili kijiweni, kila mtu akabaki mdomo wazi asiamini kama ni kweli. Sasaivi simlaumu sana huyu dem kwa maana moja kuu, mwenye lengo la kulinda afya yako ni wewe kwanza kabla ya mwingine. Mwenye maambukizi ya UKIMWI ana haki ya kuwa na mtu kimahusiano, swala la kusema hali yake ni lingine. Kuepusha hili kila mtu ajilinde, usisubiri mtu asimamie afya yako. Wenye virus hawapendi kujiweka wazi kwa kuhofia unyanyapaa lakini tamaa za mwili ziko pale pale.

Tujilinde tusisuburi watu watulinde, tuache kulaumu watu kwa uzembe wetu.

Wasalaam.
 
Back
Top Bottom