Huu siyo ukatili wa kijinsia kweli?

Huu siyo ukatili wa kijinsia kweli?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Mshangazi kanikwida nakunipiga kama mwanae katumia unene wake kama siraha dhidi yangu, kanilalia nikashindwa kuinuka akaanza kunipiga makofi ya mgongo hachagui, nilipojitahidi kuinuka akanizoga kwenye kona huku amenikaba vilivyo!

Akaona haitoshi kwa kutumia kiganja chake kinene akaamua aumize mali zangu za asili na akaniita mimi "zwazwa". Kisa cha haya yote alifuma meseji ya mwanamke mwengine na nikashindwa kuitolea ufafanuzi ulioeleweka!.

Hata hivyo sijapenda kwa alichokifanya huu ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu! Nafikiri anafaa kabisa kukutana na vyombo vya sheria sema naona aibu nitaonekana janamume lisilona staha!

Kwani kile chombo cha haki za wanaume kimefia wapi, sio kwa maumivu haya amening'ata mpaka kwenye mbavu.
 
Alafu huyo shangazi akikusumbua unahama, simple tu, hawezi kukutesa hivi
 
Back
Top Bottom