Huu usaili wa kada za afya una walakini na unatengeneza mianya ya rushwa

Huu usaili wa kada za afya una walakini na unatengeneza mianya ya rushwa

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nimesikitishwa hii mitihani kutofanyika online badala yake wanafanya mtihani kwenye makaratasi.

Kada nyingine zimekuwa zikifanya mtihani online na kwa kiasi kikubwa ni mitihani inayoaminika zaidi kuliko hii ya makaratasi.

Tatari kumekuwa na hofu kuwa hizi nafasi huenda zina wenyewe na wengine ni kama wasindikizaji tu.Kusema kweli walio na nafasi kidogo wameanza kukusanya nguvu ya fedha kwa ajili ya kutoa chochote.

Iwapo lengo ni kuwezesha baadhi ya watu kupata nafasi hizi ni bora mngewapa tu kimya kimya kuliko kuleta mfumo huu uliojaa janja janja unaokatisha tamaa.

PIA SOMA
- Usaili kada ya Afya utaanza Septemba 2 mpaka 9, 2024
 
Maisha yanaenda spidi sana leo kada za afya wanalilia ajira? Na bado watu wanazaana kama kumbikumbi!!!!
 
Mkuu acha kujiroga na hizi mentality....fanya interview kwa weledi utafanikiwa. Acha kuanza kuiumba hatima yako.

Wewe ni mwanaume, songa mbele kijeshi.
 
Nimesikitishwa hii mitihani kutofanyika online badala yake wanafanya mtihani kwenye makaratasi.
Kada nyingine zimekuwa zikifanya mtihani online na kwa kiasi kikubwa ni mitihani inayoaminika zaidi kuliko hii ya makaratasi.

Tatari kumekuwa na hofu kuwa hizi nafasi huenda zina wenyewe na wengine ni kama wasindikizaji tu.Kusema kweli walio na nafasi kidogo wameanza kukusanya nguvu ya fedha kwa ajili ya kutoa chochote.

Iwapo lengo ni kuwezesha baadhi ya watu kupata nafasi hizi ni bora mngewapa tu kimya kimya kuliko kuleta mfumo huu uliojaa janja janja unaokatisha tamaa
Mpunguze kulalamika usaili unafanyika ili kuleta ufanisi na sio vinginevyo, hizo fikra za watu fulani inaweza kufanyika tena huko online ndio rahisi zaidi

Ukiona mtu analalamika ujue hajiamini na hana uwezo kichwani

Kesho mtataka hadi fani ya kuchora pia wafanye online
 
Umaarufu, Pesa, connection,akili kubwa, Bahati.
Bila kuwa na kimoja hapo ni kupoteza muda hutapata government post.
 
Acha kulia kulia! Utumishi wapo fair sana! Achana na mentality za rushwa kijana! Ukifanya vizuri nafasi utaipata tu! Malalamiko ya nini?? Mitihani ya online ni migumu kuliko hiyo ya kuandika kwa tarifa yako! Pale dodoma watu wamepiga paper kibao na wametoboa kikubwa weka imani mkuu
 
Kwanza mimi sio dogo na sitarajii ajira hizi zinazotolewa sasa hivi,lakini kusema mitihani ya online ni migumu haiwezi kuwa hivyo kwa wote.Iletwe hiyo kisha watakaofaulu ndio waajiriwe
 
Maisha yanaenda spidi sana leo kada za afya wanalilia ajira? Na bado watu wanazaana kama kumbikumbi!!!!
Tatizo kuna mifumo imetengenezwa kuzuia kujiajiri ama kuzuia ubunifu katika kujiajiri ndio maana watu wengi wanasubiria ajira za serikali.
 
Back
Top Bottom