Huu utafiti jamani-Eti 80% ya wanaume husaliti ndoa zao……!

Huu utafiti jamani-Eti 80% ya wanaume husaliti ndoa zao……!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Imebainika kiutafiti kwamba wanawake wanne kati ya kumi huwa wanatoka nje kwenye ndoa zao. Idadi hiyo hata hivyo inaongezeka haraka sana, na inawezekana idadi hiyo ikafikia wanawake watano kati ya kila kumi. Kwa upande wa wanaume inaelezwa kwamba, kati ya kila wanaume kumi, sita au saba wanatoka nje ya ndoa zao…………duh! Nashukuru mie simo.

Kwa ujumla takwimu hizi zikikokotolewa, zinaonesha kwamba, kwenye kila ndoa kumi, ndoa nane zina mwanandoa mmoja kati yao ambaye anatoka nje au aliwahi kutoka nje. Kwa hiyo, hivi sasa ulipo hapo kwenye ndoa yenu, jaribu zoezi hili. Hesabu ndoa kumi za watu unaowajua ambao wameoa au kuolewa. Kati a ndoa hizo ni ndoa mbili tu ambazo zina wanandoa ambao hawatoki nje ya ndoa zao. Je ni wewe au mpenzi wako ambaye ni miongoni mwa hao watu wanne waadilifu? (haki ya Mungu Mtambuzi leo nitasutwa).

Hii ina maana kwamba, watu hutoka nje sana kwenye ndoa zao kuliko inavyodhaniwa. Mnaweza kudhani idadi hiyo ni kubwa sana, lakini tafiti karibu zote zilizofanywa kuhusu suala hili zinaonesha ukweli huo. Kama kwa wanawake kwa mfano, wale walioajiriwa kiwango chao cha kutoka nje ni karibu sawa na kile cha wanaume.

Hii ina maana kwamba, mpenzi wako, mkeo au mumeo yuko kwenye hatari ya kuzini muda wowote kulingana na mazingira yaliyomzunguka.
Jambo ambalo wapenzi, wachumba au wanandoa wanapaswa kulifahamu ni kwamba kuna sababu tofauti na nyingi zinazosababisha wenzetu kutoka nje.

1. Kuna kutoka nje kwa sababu watu hawako karibu tena, hakuna ule moto wa awali. Tunasema upendo umeisha au moto umezimika.

2. Kuna wale wanaotoka nje kwa sababu wanataka kuonesha kwamba, wanamudu. Kwa baadhi ya watu kutongoza na kukubaliwa au kutongozwa na kukubali, kunaonesha kwamba, mtu ana thamani, anamudu na anapendwa na wengi.

3.
Kuna watu ambao kutongoza na kumpata mwanamke fulani ni suala la kushindana.
4. Kuna wanaotoka nje ya ndoa zao kwa sababu wanataka kujihisi kupendwa, wanataka kujiona wakiwa kwenye hali ile ambayo tunaihisi tunapopendwa na wengine kwa mara ya kwanza.

5.
Kuna kutoka nje ambako ni kama kulipiza kisasi. Inaweza kuwa mpenzi amemfanyia au ameshindwa kumfanyia mwenzake jambo fulani. Ili kumkomoa mwenzake huyo, hutoka nje.

6. Wanawake hasa wanakabiliwa na kutoka nje kwa lengo la kutaka kujithibitishia kwamba, wako safi bado, yaani, 'wanadai' hata wanaume nao kuna wale wanaotoka nje na kutembea na wasichana wadogo sana. Kuna wakati hufanya hivyo kuthibitisha kwamba hawajachoka na kuzeeka. Wanatamani ujana wao.

Ukweli ni kwamba kuna sababu nyingi na tofauti za kutoka nje, lakini kwa leo naona niishie hapa.

http://wordscapes.net/extramarital-affairs.htm
 
Mkuu,

hizi tafiti zinanichanganya mno.... sasa hawa 80% wote wana-cheat na nani???
 
Mimi nasema idadi haipishani sana kwa sababu wanawake wanaotoka na hao wanaume walio kwenye ndoa nao huwa wako kwenye ndoa ama mahusiano ya muda mrefu.

Kwa hiyo nadhani kiuhalisia zaidi ngoma ni droo. Tofauti kubwa iliyopo ni wanaume huwa hawako makini katika kuficha huo uzinifu wao na wanawake huwa ni waangalifu zaidi.
 
Dingi, hizi topic unaleta huku wakati maza amesafiri zinanifanya nitafakari huwa unawaza nini ukiwa umejifungia chumbani kwako! Na tumekuomba tulale humo chumbani na ww kama wakati tukiwa wadogo umekataa! Haya weeh!
Mi nakataliana na hiyo takwimu ya 70 to 80% ya wanaume hutoka nje ya ndoa. I believe ni 99.5% lakini sina data. I don't trust any man, not even the Pope himself! I don't even trust u dad, lol! Ngoja niende zangu shule mie nisije nika-Mwanasha!
 
Nimesahau, nakubaliana na hiyo sababu #5 ya wanawake kulipa kisasi...
 
I believe ni 99.5% lakini sina data. I don't trust any man, not even the Pope himself! I don't even trust u dad, lol! Ngoja niende zangu shule mie nisije nika-Mwanasha!

Sasa hao asilimia 99.5 huwa wanatoka na nani?
 
yah nakubaliana na utafiti wako mtambuzi, ofcoz yaweza kuwa ngoma droo maana wanawake wa siku izz nao mmmh!
ndio maana rate ya ndoa kuvunjika ni kubwaa mno yan iko juu sana hii yote inaweza ikasababishwa na hii takwimu!
we imagine watu wanashabikia kbs cheatin is inevitable duh! god forbid!
 
Dingi, hizi topic unaleta huku wakati maza amesafiri zinanifanya nitafakari huwa unawaza nini ukiwa umejifungia chumbani kwako! Na tumekuomba tulale humo chumbani na ww kama wakati tukiwa wadogo umekataa! Haya weeh!
Mi nakataliana na hiyo takwimu ya 70 to 80% ya wanaume hutoka nje ya ndoa. I believe ni 99.5% lakini sina data. I don't trust any man, not even the Pope himself! I don't even trust u dad, lol! Ngoja niende zangu shule mie nisije nika-Mwanasha!
Du mshapata msamiati mpya, kaazi kweli kweli...............................
Jamani hivi uzee huu, kweli nihangaike na vimwana? si nitafia kwenye utukufu, mimi sitaki tena hayo mambo, nimeshatosheka......!
 
Nimesahau, nakubaliana na hiyo sababu #5 ya wanawake kulipa kisasi...
Kuumbeeeeee............................
Itabidi sasa nisiwe namuudhi mama Ngina, inawezekana ilishakula kwangu labda...........................Mh! hata sijui?
 
we imagine watu wanashabikia kbs cheatin is inevitable duh! god forbid!

Na sio kushabikia tu, kuna wengine ukiwa na msimamo thabiti dhidi ya infidelity unaonekana eti wewe ni wa ajabu. Utasikia wanakuambia/ wanakuuliza 'sasa utaacha wangapi?' au 'kwa nini usimsamehe tu?' au kuna wengine wanakuambia kabisa 'ili mradi tu huyo anayecheat anacheat kiheshima, mimi sina tatizo'.

Wengine wanaenda mbali zaidi na kusema kuwa 'nyumba ndogo lazima imheshimu nyumba kubwa'....
 
yap wanajipa mioyo eti wanacheat responsibly, cheatin ni cheatin basi!
hakuna cha kucheat kujiheshimu wala nn!
enh shetin ametawala haswaa kweli kbs ukistick na mtu wako huna izo stuffs, wanakuona howcome kweli.... wa ajabu, wengine watakwambia huyo mwanamke anakuchezea ww basi ila mradi tu wahararishe mambo yao.
 
Kuna kaukweli kidogo...ingawa inbidi tuchanganye na zetu
 
Bora umestuka kabla hakujakucha, big up! Na uzee huo sijui nani atakupenda kama maza.
Kuumbeeeeee............................
Itabidi sasa nisiwe namuudhi mama Ngina, inawezekana ilishakula kwangu labda...........................Mh! hata sijui?
 
Utafiti unategemea ulifanyika wapi, lini, sample size ipi, na alitumia method gani kukusanya data. Hiyo link haijanipa majibu ya kutosha. Inawezekana kwa marekani ndio ila Tanzania sio, Inawezekana data alizikusanya Ohio mida ya kazi. Kuna maswali mengi ya kujiuliza
 
Back
Top Bottom