Tuwasaidieje vijana kama hawa?
Leteni mawazo.
Kwa upande wangu, maoni yangu ni haya:
Kitu ambacho tunahitaji kukisisitiza ni kuwaambia vijana kama hawa wasilazimishe lugha kama haipandi. Huenda huko anakoomba kazi wametangaza kazi kwa lugha ya kiingereza na kijana kajikamua kweli kuwapa kile wanachotaka. Kama ndivyo, kijana amejitumbukiza tu kwenye matatizo zaidi, maana hata tuseme kaitwa kwenye usaili, lugha itamwangusha tu.Njia moja wapo ni kuwahimiza vijana kama huyu kujiendeleza zaidi kielimu ikiwa ni pamoja na kunyoosha lugha.
Vyuo kama VETA navyo vingeweza kuweka module moja ya communications skills ili kuwasaidia vijana wanaohitimu pale wasije kujikuta kwenye hali kama ya huyu ambaye hata kuandika barua ya kuomba kazi ni tatizo.