Leo asubuhi kina mama wa Mtaa wa Kilungule B Kata ya Kimara, Wilaya ya Ubungo wameamka na vilio baada ya kutapeliwa na watu waliokuja kufanya mnada wa vyombo mbalimbali kama masufuria na vifaa vingi vikiwa vya kieletroniki kama simu, laptop, sabufa, pasi na vitu vingine.
Ilikuwaje?
Watu hao wakiwa wanaume kama watano walikuja na magari mawili katika eneo hilo. Wakashuka baadhi na kuanza kuuliza kwa Watu vitu mbalimbali. Maswali hayo yalikuwa kama
- Huku wauzaji wa vyombo vya mnaada wamewahi kuja?
- Je, Watu wakukopesha vyombo vya Uturuki wamewahi kukopesha mtaani?
- Wengine wakasema tumekuja kufuatilia madeni kwa waliokopa vyombo na hawajalipa
Kama ilivyo ada kina mama ndio wahanga wakubwa.
Wakajitokeza kwa wingi hasaaaa wakiwa na vimkoba vyao vyenye pesa na wao walivyoona watu wengi wakashusha vyombo vilivyo kwenye gari chini wakavipanga na mnada ukaanza.
Waliuza simu kwa bei rahisi sana, Samsung, iPhone, Vivo na zingine sikumbuki brand bei zake zilikuwa 25,000, 50,000, 70,000, hakuna aliyenunua simu zaidi ya laki.
Ikaja TV kwa laki mbili flat screen na Laptop kwa laki mbili.
Lakini cha kushangaza baada ya kufika majumbani simu hakuna iliyowaka, tv na laptop hakuna iliyowaka. Na vifaa hivyo kama simu zilikuwa zimegundishwa na gundi ya superglue vimefungwa fungwa tu maana ilikuwa ni jioni giza linaanza nahisi watu walishindwa kukagua.
Walikuwa na Cable za kufanya test lakini baadaye walisingizia kuwa betri haiwaki ili kuchomeka katika umeme.
Hii ni aina ya risiti walizokuwa wanatoa
Waliwapa watu risiti na wakatoa na namba zao wakidai watarudi, lakini namba ikipigwa wanasema kila mtu anajibu lake mara mwenye simu hayupo, simu haipatikani au kuzimwa.
Hii ni namba nyuma ya risiti yao
Sasa huu ni utapeli mpya au kuna Watu wanalizwa huko?