Huu utaratibu upo kisheria?

Joined
Oct 8, 2014
Posts
5
Reaction score
0
Habari ndugu wana-Jf!
Naombeni kuuliza kuwa,huu utaratibu kwa wajumbe wa nyumba kumi/serikali za mitaa kutoza Tsh/= 2,000 hadi 5,000 kwa barua moja kwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo, ni utaratibu halali ambao upo kisheria?na kama ni halali,mapato na matumizi ya hizi hela yanajulikana na wananchi wa maeneo husika?
Tafadhari, naombeni majibu ya haya maswali,ndugu mana-Jf!
Ahsante!
 
Wewe unaptoa hiyo hela unapewa risiti? Kama hupewi huo utaratibu haipo kisheria. Hata siso tunachimba mtaro wa maji ya mvua wanakuja kudai posho tuliwatoa mkuku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…