Huu utaratibu wa Kiserikali haujakaa sawa, ni bomu la badaye linaloandaliwa kulipuka

Huu utaratibu wa Kiserikali haujakaa sawa, ni bomu la badaye linaloandaliwa kulipuka

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
20,419
Reaction score
39,217
Habari wanaJF,

Sote tunatambua kuwa serikali yetu ya JMT ni serikali inayojinasibu kupitia katiba kuwa ni serikali isiyo kuwa na Dini kumaanisha kwamba serikali yetu haifungamani na dini yoyote.Bali watu wake ama raia wana dini zao wanazoziamini.

Kwakulitambua hilo mana masuala mengi ya kiserikali yanaendeshwa kwa mtindo wa kutoegemea ama kupendelea dini yoyote, manake dini zote ziko sawa kwenye mizani likija suala la kiserikali ama nchi kwa ujumla.

Kwakuwa nchi yetu ina raia wenye dini mbalimbali kama za ukristo (ambao una madhehebu yake mengi), uislamu, Buddha, dini za asili, wasio amini katika dini(atheists) n.k. sambamba na hilo Dini za ukristo na usilamu ndio dini zenye waumini wengi hapa nchini.

Dini zimekua ni sehemu ya maisha na tamaduni wa wananchi wengi hapa nchini na zimekuwa na mchango mzuri katika kuleta umoja,amani na ushirikiano baina ya wananchi kupitia mafundisho na maonyo mbalimbali.

Sasa hoja yangu iko hapa:

Kumekuwa na utaratibu ambao kila kukiwa na kongamano la kiserikali,w arsha ama mikutano ya viongozi wa kiserikali ama chama.

Tunajionea viongozi mbalimbali wa dini wakihudhuria kwa lengo la kuombea baraka katika mikutano hiyo.

◇Je, kuna ulazima sana wa viongozi wa dini kuwepo kwenye kila makongamano na mikutano ya kiserikali ilihali serikali haina dini?

◇Je, hatuoni kama huu utaratibu umeanza kuleta mazoea ambayo yatajenga tabia kuwa kila palipo kongamano la serikali viongozi wa dini lazima wawepo.

◇Je, mbona kama hakuna usawa wa viongozi wote wa dini na wasio na dini kuja kuwakilisha katika nafasi ya kuomba hasa viongozi wa dini za asili ama madhebebu kama buddha n.k.

◇Je, serikali haioni inawakosea na inaleta picha tofauti kwa hawa ndugu zetu wasio amini katika dini(atheists), kuona kwamba kumbe serikali inayo dini.

Nashauri:
Ni wakati sasa serikali ijikite kwenye katiba yetu ambayo imesema wazi wazi hii nchi haina dini.Hivyo hakuna haja ya kukaribisha viongozi wa dini katika shughuli za kiserikali.

Viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa na viongozi wake huko kwenye misikiti na makanosa yao Mungu anasikia maombi popote pale sio lazima waende kwenye hayo makongamano ya kiserikali.

Serikali iache kualika viongozi wa dini mana huku ni kutengeneza mazoea na tabia mpya itakayo leta tafrani siku zijazo.

Mazoea haya yatafanya dini baadhi zijione zina thamani kuliko zingine ndani ya nchi, hii sio sawa.

Na kama mnaalika viongozi wa dini alikeni imani zote zije ziliombee taifa kama dini za asili n.k acheni ubaguzi kwa kuelemea ukristo na uslamu tu kupewa maiki kuliombea taifa pekee yao.

Mjumbe hauwawi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 2248130
 
Tumeiga serikali, tumeiga dini.

Tumeiga serikali bila dini.

Halafu tunavungavunga tu.
 
Yaani unataka mrithi wa Kingunge Ngombale Mwiru aalikwe kwenye shughuli za serikali akaombe mizimu ya Taifa naye mbele ya Rais wa JMT?
images.jpeg

Au Masanja akapige neno nae?
 
Back
Top Bottom