Huu utaratibu wa klabu kubadili jina uangaliwe upya

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Nimekuwa nafadhaika mno kwa kusikia timu inapofanikiwa kucheza ligi kuu hapa nchini inabadili jina.

Utakuta timu imepigana kwa jina lake halisi inapofuzu tu kuingia ligi kuu unasikia inabadilishwa jina na pengine kutamkwa Kiinglishi.

Nashauri utaratibu huu urekebishwe.
 
Huo mfadhaiko wako ni wa kujitakia. Maana timu haikuhusu, wamiliki wake wameamua kuibadilisha jina kwa sababu zao binafsi! Ikiwemo umiliki, udhamini, ufadhili, nk!
Wewe unafadhaika na kughadhabika!! Bila shaka utakuwa na tatizo mahali.

Na kama umechukizwa sana na huo utaratibu, basi na wewe anzisha timu yako ya mfano! Halafu ipambanie ipande mpaka ligi kuu! Na ikifika katika hiyo hatua, iache tu ibakie na jina hilo utakalo litumia kuanzia pale ulip ianzisha! And no one will ask you for anything.
 
Punguza ghadhabu mkuu.
Mfano, Kitayose nasikia inabadilishwa jina kwa kuiita Tabora United ambayo ipo tayari ina imeshindwa kupanda daraji.
Sasa jiulize historia ya Kitayose itaishia wapi?
 
Punguza ghadhabu mkuu.
Mfano, Kitayose nasikia inabadilishwa jina kwa kuiita Tabora United ambayo ipo tayari ina imeshindwa kupanda daraji.
Sasa jiulize historia ya Kitayose itaishia wapi?
Hiyo ni biashara mtu anaipandisha timu kisha anaiuza kwahyo aliyeinunua anabadilisha jina mfano DTB ilivyopanda tu ikauzwa na kuitwa Singida Big stars na hadi makao makuu ya club yakahama
 
Iko hv huu utaratibu ulipitishwa Kwa namna ya kuviokoa vilabu vinavyo pitia Hali ngum ya kiuchumi n.k.
Sasa basi wakapitisha Ili kusaidia hilo club inaweza uzwa na mnunuaji akawa na haki ya kubuni jina lake Kwa mapenz yake na hata kuihamisha makazi na kuelekea mahali anapopataka yeye Kwa kufuata utaratibu ulowekwa .

Mfano mmsimu huku championship zinakopambana team Ili zipande ligi kuu, huku ndo kutamu unakuta team imebakisha match5 tu imalize msimu na kama akishinda match 3 tu anafuzu kuingia ligi kuu ila wanapitia wakati mgum WA kiuchumi hawawezi safari hvo kuamua kuiuza na ndipo ndugu matajiri wanapata mserereko na kununua haki zote kuanzia club Hadi jina na mahali.
 
Kubadili jina Sawa lakini kuhama makazi wasiruhusu
 
HILI NALO MKALITAZAME!

Halafu kuna hii tabia imezuka timu ikiboronga inabadilishwa jina mfano simba fc siku hizi inaitwa MAKOLO
 
Wabongo bhana sasa unaumia kitu gani?
 
Kubadili jina ni ujinga tuu , hata walioipandisha timu daraja wanatengwa , na kuonekana hawafai wanatokea wajuaji wengine mwisho timu inashuka tena daraja na jina lake jipya.....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…