Huu wimbo wa Simba ni majanga

Huu wimbo wa Simba ni majanga

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Me binafsi ni mshabiki wa Simba lakini kuwa kwangu mshabiki wa Simba hainizuii kuwa mkweli kiukwel huu wimbo wa Simba ni mbaya lakini wasanii walioimba mrisho mpoto na tundaman walikuwa hawana chemistry kabisa hiv kwel mmekosa wasanii wakuwapa project yenu mpaka mnawapa tundaman na mrisho mpoto watengeneze hitsong serious? Huyo aliyeruhusu huu wimbo uwe wa club Basi atakuwa wale wale wa 10%.Yaani ngoma hata aistui haina mzuka haina Melody nzuri ya kufanya msikilizaje aufurahie hiv sisi tunafeli wapi? Wenzetu wazungu suala la song la club wanachukulia serious kabisa ndo maana wanatengeza nyimbo nzuri mfano wimbo wa real Madrid ni mzuri Sana kuusikiliza ingawa sijui wamezungumzia Nini? Ebu tujiulize huu wimbo wetu wa club unaweza ukausikuliza kwel hata mshabiki ambaye si wa Simba akaupenda kweli?
 
Ilikuwaje mpaka wampe Mrisho Mpoto?
Sijausikia lakini tayari wameshanitoa stimu.

Bora hata wangewapa wapiga Singeli.
 
Bora mtumie tu ule wimbo wa msimu uliopita wa Msaga sumu! ulikuwa una amsha amsha.Mimi ni Yanga! lakini ile simba day yenu iliyopita, hakika ilifana sana kupitia ule wimbo.

Sasa Mrisho Mpoto na kuimba wapi na wapi! Huyo Tundaman mwenyewe huwa haeleweki anachoimbaga zaidi ya kulialia tu.
 
Mwaka huu Simba day haiwezi kuifunika wiki ya mwananchi...hakuna tukio kali kama wachezaji walivyoizunguka nembo ya klabu..iga tembo kuny@......
 
Kwani mkuu umesikia Tundaman kalipwa sh ngapi mpaka unazungumzia 10%?
 
Bora tungefanya mazungumzo na TWANGA.... tuutumie ule utunzi wa marehemu BANZA STONE km wimbo rasmi wa team!
 
Katika hili wana msimbazi tumeshalilishwa pakubwa
 
Back
Top Bottom