Huu wizi TCRA hawajawahi kuusikia au kuna ujanja unafanyika?

Huu wizi TCRA hawajawahi kuusikia au kuna ujanja unafanyika?

Vanlizerfx__

Senior Member
Joined
Jul 7, 2021
Posts
114
Reaction score
191
Kama uliwahi kuweka vocha kwenye simu yako alafu ukakuta ile hela uliyoweka haipo na wala hujaitumia, ulishawahi jiuliza inaenda wapi nini kifanyike ili kuzuia wizi wa namna, nini kinafanyika kuzuia wizi wa aina hiyo.

“Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanapoteza pesa kujiunga na vifurushi ama wanaponunua vocha… Serikali itachukua hatua gani kudhibiti Makampuni ya simu ambayo yanafanya wizi kwa wananchi”

Ina maana TCRA hawajasikia haya malalamiko?
“Kumekuwa na udhaifu mkubwa kwa upande wa TCRA kwenye kufuatilia malalamiko ya watu pale ambapo wanadhurumiwa, watu wanatoa malalamiko kwa Makampuni ya simu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa”

Au tuseme maboss na wafanyakazi wenye vyeo vikubwa TCRA wanahusika na kula rushwa na kufumbia macho swala hili??
 
Back
Top Bottom