Huwa inashangaza sana

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Hichi kitu huwa kinanishangaza sana ikitokea mtu ukiwa unapost habari kuhusu wasanii watu wanakuita mbeya lakini ukitoa habari za wanasiasa hauitwi mbeya , tuchukulie mfano juzi magufuli alienda kumjulia hali mkewe hospitali ile habari ililetwa humu na kujadiliwa bila kujali kwamba suala hilo ni maisha binafsi ya magufuli na mkewe LAKINI nina uhakika habari hiyo hiyo ingeletwa mfano Diamond ameenda hospitali kumjulia hali Zari ,mtoa mada angeitwa mbeya ,sasa nataka mnifahamishe tatizo ni nini?


Pia ikitokea mwanasiasa hajahudhuria sherehe au msiba wa mwanasiasa mwenzake hii habari ikiletwa humu haitaonekana ya kimbea lakini kama msanii hajahudhuria msiba wa msanii mwenzake au harusi ,hiyo habari ikiletwa humu utaitwa mbea mfano kipindi kile mpoki alivyokosa kuhudhuria harusi ya masanja na hiyo habari ikaletwa humu mleta mada alionekana ni mbea sana lakini labda ingekuwa hivi " Mh Hussein Bashe apata jiko lingine lakini swahiba wake HAMIS kigwangala hakuhudhuria harusi" hii habari isingeonekana ya kimbea



Najua watu wengine watakuja na hoja nyepesi wakidai wanasiasa ndio mhimili wa taifa hivyo wanapaswa kuzungumziwa muda wote
 
mkuu mim kwa upande wangu nadhani..watu wakubwa au famous wanaoangaliwa sana kwa kipind hiki ni hao wanasiasa especially rais,vice,spika,ns na mawaziri kulingana na serikali iliyopo saiv hao ndio watu wamekaa sana midomoni mwetu pia wanafuatiliwa kwa ukaribu zaid,na wananchi humu ndani kwasababu wana impact kubwa au kulingana na hali ilivyo na sio kwamba ikija habari imeletwa kuwa rais kaenda kumtmbelea mkewe hospital mnh basi habar itajadiliwa ivo hapana inajadiliwa kwa mapana yake na mambo mengi zaid sababu humu kuna great thinkers so jarbu kufatilia hta kam ni lada wazir fulani kaoa watu hawatachangia uzi kuhus harusi yake no,kuna mengi nje na hilo kubwa watajadili.so ndo iko ivo mkuu
 
Usisikilize ya watu wewe tuletee habari.
haya ndo maneno sasa dada yangu maana kuna mtu najuana naye lakini nilikuwa sijui kuwa yeye ni member wa humu JF lakin siku moja akawa anazungumzia habari za humu ,nikamuuliza username yake humu JF ni nan akantajia lakin ilikuwa ngeni kidogo username yake nikamwambia swahiba hili jina geni kabisa maskioni mwangu akaniambia kuwa yeye hayupo kwenye majukwaa ya umbea umbea nikawa nashangaa kwa nini celebrities forum aliite forum la wambea nikashindwa kumuelewa kwa kweli

Pia utakuta wanaoleta habari za wanasoka hawaitwi wambea ila wanaoleta habari za wanamuziki wanaitwa wambea hapa ndo naashindwa kuelewa kabisa
 
Wanaoleta habari za wasanii ni wambeya, wanaoleta habari za wanasiasa wamwanza, wanaoleta habari za Football ni wabrazil ndio hivyohivyo wanaoleta habari za urojo ni wapemba. Upo hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…