Huwa unadhibiti na kulinda vipi Taarifa zako binafsi?

Huwa unadhibiti na kulinda vipi Taarifa zako binafsi?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Siku ya Faragha ya Taarifa huadhimishwa Januari 28 kila mwaka ikiangazia kuongeza uelewa kuhusu masuala ya ulinzi wa taarifa binafsi na kuhimiza sera na kanuni bora za kulinda taarifa za watu katika ulimwengu wa kidigitali

Pia, siku hii inalenga kuwawezesha watu kufanya maamuzi sahihi ya kulinda taarifa zao na kushinikiza maboresho ya sheria za faragha

Kauli mbiu ya mwaka huu “Chukua Udhibiti wa Taarifa Zako,” inalenga ikiwakumbusha watu kufanya maamuzi sahihi kuhusu taarifa zao

====== For English Audience======​

Data Privacy Day 2025: Date, History, and Theme
In 2025, Data Privacy Day is observed on , January 28th, under the theme, “Take Control of Your Data,” which serves as an assertive reminder for people to make informed decisions about their data and information.

This day promotes awareness of data protection issues and encourages best practices and regulations for protecting individuals’ data in an interconnected society.

Data Privacy Day is a critical event in the digital era, emphasising the need to safeguard personal information and ensure data-handling procedures adhere to privacy and regulatory requirements.

It enables people to make more educated decisions about their data and pushes for improved privacy laws.

Screenshot 2025-01-28 142500.png


Robert Majige
Tech & Media Convergency (TMC)

Tunatarajiwa kuwa na mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu elimu ya Akili Mnemba (AI), kwa nini tumewachagua Wanahabari? Ni kwa sababu kupitia wao wanafika kwa Watu wengi na inaweza kuwa rahisi kuwafikia watu wengi.

Kuna umuhimu wa watu kujua kuhusu na matumizi sahihi ya Akili Mnemba na pia tansia ya Habari ni moja ya sekta ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya AI.

Screenshot 2025-01-28 163524.png
Tryphone Rwezahura
Afisa wa Sheria, JamiiForums

Social Media ni njia ya kusambaza taarifa mbalimbali lakini maendeleo ya teknolojia yamechangia pia kuwepo kwa taarifa nyingi potofu.

Kupitia JamiiForums tuna Jukwaa la JamiiCheck ambalo linajihusisha kuhakiki taarifa ambazo zinaonekana kuwa na mashaka, mfano wa taarifa hizo ni zile ambazo zimekuwa zikitengenezwa na Akili Mnemba (AI).

Mbali na hapo tumekuwa tukiwafundisha watumiaji mbalimbali matumizi ya sahihi ya AI, tumekuwa tukitoa darasa hilo kwa wadau tofauti wakiwemo Wanafunzi, Wanahabari, Watumishi wa Serikali na hata Watumishi wa Sekta binafsi.

Tumetoa elimu hiyo pia mara nyingi kwa njia ya kukutana na ha hata njia ya Mtandao.

Unaweza kuwa mmoja wa watu ambao wanajihusisha na utoaji wa taarifa sahihi au kuomba kufahamu usahihi wa taarifa kupitia JamiiCheck.com ambapo pia unaweza kulipata jukwaa hilo kupitia JamiiForums.com

Screenshot 2025-01-28 152519.png

Fatma Songoro
Head of Technology Law Department (Victory Attorneys & Consultants

Wanasheria tunatakuwa kubadilika kulingana na uhalisia wa maendeleo ya teknolojia, kumekuwa na dhana kuwa tasnia ya Sheria au Wanasheria ni watu ambao ni wagumu kubadilika au kukubaliana na mabadiliko.

Wanasheria wao ndio wanatakiwa kuwa njia sahihi ya kuwaonesha wapi Wateja wao wanatakiwa kuelekea katika upande wa masuala kama ya AI.

Tryphone Rwezahura
Afisa wa Sheria, JamiiForums

Ukusanyaji wa Taarifa Binafsi ni jambo ambalo watu wengi wanatakiwa kuwa makini, unapompatia mtu taarifa zako muhimu huweze kujua atazitumia kwa njia gani, vipi kama akitumia vibaya dhidi yako?

Tunatakiwa kuwa na njia sahihi ya utoaji wa Taarifa Binafsi na kutambua unampatia nani na kwa matumizi yapi? Hayo ni maswali ya msingi ambayo tunatakiwa kujiuliza na kutambua umuhimu wake.

Robert Majige
Tech & Media Convergency (TMC)

Tunahitaji kuwa na kitu kama Bodi kwa ajili ya matumizi ya AI, ambapo inaweza kuratibu na kudhibiti matumizi yasiyo sahihi kwa ajili ya akili mnemba ndani ya nchi.

Kama tumeweza kuwa na bodi ya masuala mengine mengi ya msingi nadhani ni sahihi pia tukawa na utaratibu maalum wa kuratibu matumizi sahihi ya AI.
Screenshot 2025-01-28 153947.png
 
Back
Top Bottom