Huwa unazishindaje dharau na chuki dhidi yako zinapoibuka?

Huwa unazishindaje dharau na chuki dhidi yako zinapoibuka?

Mia saba

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
255
Reaction score
390
Ni rahisi tena mno kuona watu wakisambaza maneno ya chuki kwa jamii juu ya watu fulani hivyo hupelekea watu hao kujidhuru kwa kushindwa na maneno ya dhihaka.

Kama mwana jukwaa huwa una mbinu gani juu ya watu wanaokuletea dharau, majivuno na chuki.

Let's share ideas.
 
Maneno mengi tumesingiziwa.

Mwili umejaa makovu.

Yataka ujasiri kushinda vitu hivyo.
 
Kuna mmoja namnyoosha kimya kimya.
Nimechagua njia ya kutegua mabomu.

Alianza kusambaza maneno eti namchukua mke wa jamaa..jamaa akanichukia mimi sijui. Nilipozipata siku hiyo hiyo nikamfata jamaa nikamuelewesha na vielelezo na ushahidi wa jinsi mzushi anavyocheza mchezo wa kutugombanisha,saizi peace halafu jamaa na huyo mzushi maji na moto.

Juzi Kati yule yule kazusha maneno mengine, nilipoyanyaka nikamfata mhusika tena, nikamuelewesha..peace halafu wao saizi kama serikali na bhange.

Simple like that!!!!
 
yaaan nimefikia level ambayo hata nisingiziwe jambo lolote kubwa moyo wangu haushituki, mtu akiniletea dharau na kiburi mwsho wa siku huanza kulalamika yeye kwamba mimi nina jiona nina ringa... Inshort najua kupuuzia mtu hata awe amenizidi kwa kilakitu lakin lazima atajiona hana thamani.

Sikuzote jifunze KUPUUZIA watu ambao wanajiona wao ni bora kuliko wewe, ukiweza hili hata awe na nguvu au cheo utamuona ni ng'ombe tu kama ng'ombe wengine...
 
yaaan nimefikia level ambayo hata nisingiziwe jambo lolote kubwa moyo wangu haushituki, mtu akiniletea dharau na kiburi mwsho wa siku huanza kulalamika yeye kwamba mimi nina jiona nina ringa... Inshort najua kupuuzia mtu hata awe amenizidi kwa kilakitu lakin lazima atajiona hana thamani.

Sikuzote jifunze KUPUUZIA watu ambao wanajiona wao ni bora kuliko wewe, ukiweza hili hata awe na nguvu au cheo utamuona ni ng'ombe tu kama ng'ombe wengine...
Kuna mzungu mmoja anatabia yakunipita tu bila kunipa salamu na hajawahi kunisemesha hata siku moja sasa kunasiku kapita sijui anaenda kufanyeje uko anajua mwenyewe kumbe njiani alipotoka kuna watu wanamdai pesa naisi walikuwa mafundi kumbe walikuwa wanamdai walivyo Kutana wakaanza kupigana, yule mzungu akaenda kushtaki polisi kwamba kapigwa, polisi wakamwambia apeleke mashaidi sasa alivyokuwa mjinga akanifata mimi niwe shahidi yake sasa mimi nikajiuliza huyu anisalimiagi ananionaga kama takataka leo hivi kapata tatizo ndiyo ana jifanya kunisalimia, sasa namimi nikawa simjibu akiniongelesha najifanya nipo Bize na saingine nikimuona tu namuangalia kama takataka, uzuri wake na yeye kashajua.
 
Wengi wamependekeza PUUZA.
Nakubaliana nao,maana wengi hutaka kuona utafanya nini,sasa wewe uwakwepa wasijue nini utafanya.Hii lazima imuumize kila mpuuzi!
Tatizo la dharau/manyanyaso ni kubwa ktk jamii yetu na mbaya zaidi mtu anataka amnyanyase mtu mzima mwenzie bila kujari utu uzima wa muhusika!
 
Heshima ni kitu cha bure.
Lakini kwangu kama uniheshimu na sijui wala hunioneshi ni sawa tu ila kamwe usijaribu kunionyesha dharau zako mbele yangu tena direct kwangu hapo utakuwa umechokoza vita, ni simple tu inakuwa vita ya tatu ya dunia bila kupepesa macho. nakufata machoni alafu nakwambia wewe mbuzi usinizingue na ukiendelea kuniletea mambo ya kifala basi dunia utaiona chungu na ya moto.

Iko hivi ni eidha utaniheshimu kama ukishindwa kuniheshimu basi utaniogopa na kama ukinishindwa kuniogopa basi utakaa mbali na mimi na kuniacha na maisha yangu na ndicho ninachotaka. tunaenda kidiplomasia au kibabe hakuna kulialia na kuoneana maisha yenyewe mafupi. simple, short and clear.

Mimi sio mkorofi lakini siku zote nasema hakuna kuwa mstaarabu mbele ya washenzi au utakufa kwa stress, kuwa mstaarabu na civilized mbele ya wastaarabu na kuwa mshenzi mbele ya washenzi.

Kitaalamu inaitwa environment adaptability and flexibility. or suffer and die.
 
Back
Top Bottom