Benittotz
Member
- May 24, 2018
- 68
- 123
HUWEZI FANIKIWA KWA NDOTO ZA MWINGINE, KUWA DEREVA KAMILI WA MAISHA YAKO.
Hivi umewahi kujiuliza ingekuwa vipi kama ungeijua siku yako ya mwisho duniani? Je! Ungeendelea kuishi na kutenda Kama ufanyavyo sasa? Ungeendelea kuweka ndoto zako kiporo na kwa kisingizio cha "nitafanya kesho" kesho hivi,kesho vile?.Sasa mbona haijui kesho yako lakin Wala haushtuki? Miaka inasonga na uzee unakaribia. Ndoto nyingi zinayeyuka na bado umetulia ukisubiri mambo yawe sawa ndio uanze kutimiza ndoto zako,rafiki yangu ukweli ni kwamba utaendelea kusubiri sana. Mambo hayajawai kuwa sawa hata Mara moja.
Wanasema ndoto nyingi ziko ardhini ( wakiwa na maana kwamba watu wengi wameondoka na ndoto zao kichwani bila kunifanyia kazi). Lakini hata baada ya kulijua hilo Tena kwa mifano mingi bado tunaishi Kama vile tumeahidiwa muda wote katika hi dunia. Wakati wengine wakipambana katika Hali nzuri na mbaya ili kutimiza ndoto zao wew bado upo umelala ukiendelea kuota na kuota pass kuchukua hatua. SIMAMA,JITFAKARI,WAKATI NDIO HUU.
Leo ndio ile siku unaacha kuishi ndoto za wengine na kuanza kuzijenga za kwako.Acha kula makombo ya watu wengine,kila mtu ana mpango na namna yake ya kufanikiwa kimaisha. Usiigize alichofanya fulani. Ingia jikoni andaa Cha kwako,kizuri na kwa ajili yako,hata harufu inaposikika huko nje kila mtu anajua haya ni mapishi ya fulani. Usitake kuwa daktari sababu mama amekwambia au ndugu yako ni daktari,hiyo ni kula makombo,kuwa daktari kwa sababu unapenda na ni ndoto zako. Usisome biashara sababu inalipa na jamii imekushawishi, soma biashara sababu inakupa amani ya moyo na unaiona kesho yako katika hiyo taaluma. Shikamo usukani wa gari linalobeba maisha yako na uwe dereva Kamili wa mustakabali wako.
Vipo vikwazo na changamoto nyingi katika kutimiza ndoto zako.Lakini ni bora kuamini na kujaribu, sababu usipofanya hivyo dunia itakunyang'anya ndoto zako. Itakujaza woga na hofu na kutufanya mtumwa maisha yako yote.
Zifuatazo ni baadhi ya hatua zinazoweza kukutoa katika utumwa wa kuishi ndoto za wengine,kula makombo ya wengine na kutufanya kuwa bora katika kile unachokiamini.
1.KUWA NA MAONO.
Lazima uione kesho yako. Lazima ujione unataka kuwa Nani,unataka kuwa wapi siku zijazo. Chora ramani kichwani mwako na amini katika ramani hiyo. Mwanamam mhamasishaji Vera Jones anasem "sight is physical, vision is spiritual" akiwa na maana kuwa kuona ni kimwili bali maono ni kiroho. Akazidi kusema pia "sight is perception of your present while vision is future on your faith" akimaanisha kuona ni mtazamo juu ya wakati uliopo wakati maono ni kuwa na imani na wakati ujao. Kama huna maono,Kama huioni kesho yako ni ngumu sana kuwa kuishi katika ndoto zako.
Jambo la kufurahisha katika hili ni kwamba Mara zote ni rahis Sana kujua moyo unapenda nini. Fata moyo wako. Wanasema unapofata kile unachopenda na kukifanya taamula yako basic nafasi zako za kufanikiwa huwa nyingi zaidi. Anza leo kufanyia kazi unachopenda kimbiza ndoto zako sababu wewe NI mshindi. Usiruhusu jana yako iishinde kesho yako.
2.ISHINDE HOFU.
Kama kuna kitu kinauwa ndoto nyingi basi ni hofu. Watu wengi wameacha ndoto zao zikapotea sababu ya hofu. Wakidhani pengine wao si bora au hawana uwezo wa kufanya jambo flani. Wakiogopa kuanzisha mazungumzo na watu ambao wangekua funguo katika kutimizia azma yao ya mafakinio. Usiruhusu hofu iwe kikwazo kwako. Unaogopa nini hasa? Kwanini uogope? Hao unaowaogopa wana maisha yao na wanakimbiza ndoto zao hawana muda wa kuangalia kama utaanguka ukijaribu ama la. Vaa ujasiri,simama najiambie wewe ni bora na unaweza kisha toka na uanze safari yako yamafanikio kwa imani na tabasamu. Mwandishi Robert Kiyosaki anasema "when you lose,lose big and when you win,win big" ( Kama unashindwa shindwa kwa kishindo na kama unashinda shinda kwa kishindo)
Akazidi na kusema watu wa Texas,Marekani wanamsemo wait kuhusu hofu,wao husema "when I win I am proud, when I lose I brag" wakimaanisha "ninaposhinda naona fahari na nikishindwa najigamba" Hata wewe huna sababu ya kuogopa kushindwa, ukijaribu na kuanguka hujarudigi nyuma umeanguka kusogelea sehemu bora zaidi. Wewe ulieanguka katika kukaribia mafanikio ni tofauti na yule ambae hajawahi kuanguka kabisa. Wewe tayari umejenga msingi,umeyajua makosa na njia za kuyatatua kuamka kwako kutakua kwa kishindo. Usiwe na hofu ukiamini lazima utatimiza. Mwigizaji Will Smith anasema "katika kilele cha hofu ndipo penye kilele cha kujiamini" Ukiona unaogopa sana jua wewe ni jasiri pia. Simama mbele ya kioo na ujikumbushe dhamira yako utakuwa upande wa pili wa ushindi,upande wa ujasiri na upande wa kufanya maajabu.
Kamwe usiruhusu hofu ikufanye mateka wa kula makombo ya wengine, ingia jikoni ujipikie mwenyewe Kama wao hawakuungua hata wewe hutaungua na moto.
3.ANZA KUTEMBEA.
Leo ndio ile siku unapaswa kuanza kuhudhuria darasa la mazoezi ili upungue au kuongezeka na kupata ule mwili unaoutamaini kila siku. Leo ndio ile siku unapaswa kuanza kujifungia chumban kujisomea ili kupata yale matokeo unayoyatamani kila siku katika dunia yako ya kitaaluma. Na leo ndio ile siku unaenda kuacha iyo kazi yenye mshahara mdogo, mazingira mabovu na inayokupa msongo na madeni kila kukicha dukani kwa mangi. Unaenda kuanza upya maisha yako,kupiga hatua chanya kuelekea katika ushindi. Mwimbaji Tatiana Manaos aliimba akasema "you got to wake up and make a move, cause the world will never see you until you do". Akimaanisha "unatakiwa usimame na upige hatua,sababu dunia haitakuona mpaka utakapo fanya hivyo"
Fanya tafiti,wapo watu wanaofanya na wameshafanikiwa katika kile unachotaka kufanya. Watazame,chunguza walipoanzia, changamoto walizokutana nazo,walizishinda vipi. Kisha tengeneza njia yako na uanze kutembea.
DONDOO NNE ZA KUFATA ILI KUPIGA HATUA
i) Chagua mafanikio. Kabla ya kuanza kupiga hatua yoyote ile lazima uwe umechagua ushindi. Jiepushe na kataa misemo Kama vile "mimi bado mdogo umri ukifika nitafanya" " nikipata hell ndio nitakua nifanye Nini" "kuwafanikiwa ni mateso Sana"
Kuwa na imani chanya itakayokusukuma kufikia lengo lako.
ii) Wekeza katika elimu,ujuzi na maarifa ya kile unachotaka kufanya. Hii ni nyenzo muhimu zaidi kufikia ndoto zako. Ukiwa na ufahamu wa kutoshaa kuhusu unachotaka kufanya ni rahisi kufanya kwa fanisi na leave mafanikio.
iii) Chagua marafiki. Hapa sina maana uchague marafiki waliofanikiwa au went malengo kama yako tu. La hasha. Chagua marafiki wa aina zote. Wale waliofanikiwa watakufunza zaidi kuhusu mafanikio na namna gani ya kufika huko. Na wale wasio na mafanikio watakufunza kitu gani usifanye ili usikwame Kama wao.
iv) Jifunze kila siku. Kujifunza hakuna mwisho kila utakapo pata ufahamu kuhusu jambo moja ongeza ufahamu kuhusu lingine.
4. KUWA MNYENYEKEVU.
Kuna wakati unapaswa kukubali kutojua jambo fulani na kuomba msaada kwa wanaojua. Angelo Maya anasema. " Nimegundua no kiasi gani sifahamu" hii kauli inapaswa kuishi ndani yako Jifunze kila wakati toka kwa waliokutangulia. Vera Jones anasema " when pride says do it yourself,and wisdom says ask someone who knows, you better listen to wisdom. You will not regret" . Akiwa na maana kuwa "wakati nafsi ya kiburi inakwambia unaweza, na busara ikakwambia muulize anaejua,ni vyema ukaisikiliza busara. Hutajutia". Hivi ndivyo ilivyo siku zote hakuna mtu aliejitengenezea mafanikio yeke pekee yake wazungu wanasema "self-made". Niamin nachokwambia hakunaga kitu Kama self-made duniani. Katika kukua kwetu Kuna watu nyuma yetu siku zote watu ambao aidha moja kwa moja au kwa namna nyingine wamehusika na ukuaji wetu na ukuaji wa ndoto zetu.
Hivyo basi ndugu msomaji wakati wako ndio huu,wakati wa wewe kuacha kula makombo. Wakati wa wewe kuacha kuilalia ndoto yako na kuendelea kuburuzwa na dunia. Huu ndio wakati unaacha kujichukulia poa na kuwa tolea Bora la wewe sababu wewe ni mshindi na umezaliwa kufanya Mambo mambo makubwa. Si tuu kwa ajili yako Bali kwa jamii iliyokuzunguka na dunia kwa ujumla. Hatupewi karama zituufaishe wenyewe tunapewa kwa makusudi sababu kupitia karama zetu wapo watakonyanyuliwa. Hivyo kulalia ndoto zako sio tu kujidhulumu,unaidhulumu jamii yako na kumkosea Muumba wako aliekubariki na kipawa hicho. Amka sasa pigania Uhuru wako.
Ni imani yangu kuwa katika makala hii fupi Kuna Jambo moja au mawili umejifunza. Na hata yale uliyokuwa unayafahamu tayar labda umeyepokea kwa sura nyingine Tena.
Ningependa kusikia kutoka kwako,ukinishauri,kunikosoa na kurekebisha pale unapoona sikuwa sawa au kuongeza jambo. Lakini pia napokea mapendekezo kutoka kwenu,ni mada gani hasa ya kiuchumi mngependa niandike kwa ajili yenu.
Na
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAMU SHULE YA BIASHARA
FACEBOOK: Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz.