Adili Utotole
Member
- Jul 20, 2022
- 14
- 14
Ajira ni kazi yeyote anayoifanya mtu na kulipwa ujira kwa makubaliano maalumu. Au ni kazi aifanyayo mtu inayoweza kumuuingizia kipato. Kuna aina kadhaa za ajira. Ajira binafsi, hii ni aina ambayo mtu hujiajiri mwenyewe, iwe kuuza duka, kuuza matunda au ufundi seremala, bomba na umeme.
Ajira isiyo rasmi, au ajira ya muda mfupi. Aina hii hufanywa na watu wasio na mikataba maalumu,tunawaita Vibarua.Mtu hupokea malipo kulingana na muda wa kufanya kazi, Mara nyingi hutegemea posho Kama ndio malipo yao.
Pia kuna ajira za muda mrefu, hizi ndizo ajira rasmi, mtu hupokea malipo kulingana na maelekezo ya mkataba wake. Mara nyingi huwa ni ajira za kudumu pia.
Kwa maelezo ya kitengo cha kutoa takwimu Cha Statista.com walichotoa mwezi Mei mwaka huu kinasema, kuna kadiriwa kuwa na watu bilioni nane ulimwenguni kote. Na Kati ya hao watu bilioni 3.32 ndio wameajiriwa. Nalo shirika la Trading Economics linaeleza kuwa nchi ya Mexico ndio yenye waajiriwa wengi, ikiwa na asilimia 96.65. Ujerumani ni ya 11 ikiwa na asilimia 77 ya waajiriwa na Uingereza ni ya 15 ikiwa na asilimia 75.9.
Kwa Sasa tatizo kubwa ulimwenguni ni ukosefu wa ajira,hali inayosababishwa na kudorora kwa uchumi katika nchi nyingi. Tunaendelea kushuhudia wahitimu katika sehemu mbalimbali kielimu wakihaha kutafuta ajira mara wanapo maliza au kuhitimu mafunzo.
Nakumbuka miaka ya nyuma wazazi au watu walikuwa na mwamko wa kiwaaisitiza watoto jamaa au ndugu zao kuwa wasome kwa bidii ili waje kupata ajira nzuri baadae,ni kweli ajira zilikuwa ndio kila kitu kwa wakati ule tofauti na Lakini kwa Sasa huwezi kusikia kauli kama hizo Mara kwa mara,kwanza mtu asome ili aende wapi, na akafanye kazi gani?,wakati hata yule mwenye digree hana ajira anazunguuka mitaani.
Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akihitimisha ziara yake jijini Mwanza Juni 15 mwaka 2021, Mbunge wa Sengerema ,Mheshimiwa Hamisi Tabasamu alipopata nafasi ya kuzungumza alimalizia hotuba yake kwa kusema ,nanukuu "Vijana someni ,someni mkitambua kuwa tukisoma tutaelimika, tukielimika tutajiajiri wenyewe, serikalini hakuna ajira" ,mwisho wa kunukuu.
Kwa kauli hiyo ni dhahiri kwamba kuna ukosefu wa ajira. Kwa Sasa juhudi ,kipaji na nidhamu ndivyo vitakavyofanikisha kile unachokihitaji kupitia kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe.
Msingi wa andiko hili ni kwamba huwezi kufanikiwa vizuri kujiajiri kama hujawahi kuajiriwa. Wengi tumeshuhudia linapotokea tangazo au unapoomba kazi yeyote ,kigezo kinachoangaliwa ni uzoefu wako katika kazi hiyo. Wakiamini huko kuna mambo ulijifunza,hivyo hautawapa kazi ya kuanza kukufundisha upya au kukuelekeza.
PICHA JUU: TANGAZO LA KAZI LIKIELEKEZA VIGEZO VYA KUOMBEA (Picha kwa hisani ya Officialbakhresagroup kupitia Instagram).
Kuna faida za kuajiriwa kabla hujajiajiri mwenyewe. Itakuongezea nidhamu ya kufanya kazi. Tunajua kila shirika , kampuni au sehemu yeyote ya kazi ina misingi na taratibu zake. Lazima ufike kwa wakati katika eneo husika ,ukichelewa kuna adhabu zake,pia ni lazima utii maagizo mengine ya mwajiri wako.
Kama ukiwa mtu makini, msikivu ,au mvumilivu katika kazi ya mtu ,ni rahisi Sana kufanikiwa endapo utaanzisha biashara yako au itakuwa rahisi kujiajiri katika Jambo lolote. Nimewahi kuona wafanyabiashara na wajasiriamali wengi ambao biashara zao zinakufa au haziendelei kwa sababu ya kukosa uzoefu.
Fikiria hujaajiriwa popote, hauna matatizo ya kiafya ,sio mzee wala hauna ulemavu wa viungo. Lakini unaenda kuanzisha ujasiriamali halafu unatafuta wasaidizi lukuki. Hatukatai kugawana riziki , kama hakuna uhitaji wa namna hiyo kwa nini na wewe usiwe miongoni wa watendaji kazi. Biashara yenyewe ni ya kuuza duka, matunda au chakula, unanunua vitu ,tena kwa kumtuma mtu, huku wewe unaenda kulala ,Unaenda kijiweni kucheza drafti au kutembea sehemu isiyokuwa na ulazima ,ukisubiri hesabu jioni.
Wajasiriamali au wafanyabiashara wengi tunapenda kuitwa "Mabosi" .Hali hii hisababisha biashara kupungua mauzo au kufa kabisa baada ya miezi kadhaa .Wasaidizi watakuibia au kuharibu biashara kwa kukosa usimamizi mzuri.
Siku moja nilienda katika mgahawa mmoja jirani,bahati nzuri alikuwepo mmiliki mwenyewe wa biashara na msaidizi wake mmoja ,japo yule msaidizi alikuwa ameenda kupelekea wateja wengine oda. Baada ya kuagiza chakula yule mmiliki aliniambia " Msubiri msaidizi wangu ametoka aje akuhudumie" , huku yeye akiwa anaperuzi simu janja yake na mboga ilikuwa ipo jikoni inakaribia kuungua nikiisikia harufu, kwa kuwa nilikuwa na njaa nilimsubiri yule msaidizi wake mpaka alipokuja kunihudumia. Na ilikuwa kawaida ya mmiliki yule kufanya hivyo siku zote, wasaidizi walifanya kazi juma moja na kuondoka. Na Sasa biashara amefunga kutokana na kukosa wateja.
Mimi mwenyewe kuanzia mwaka 2011 hadi 2013 nilikuwa nimeajiriwa .Kwa bahati nzuri nilikuwa nakaa pale pale kwa mwajiri wangu na kijana mmoja tuliyekuwa pamoja katika kazi. Kwanza bosi wetu hakupenda tutumie kilevi chochote , nyumbani ilikuwa kurudi mwisho saa tatu usiku kipindi ambacho tulikuwa mapumnzikoni. Pia alikuwa anachukia Sana alipokuwa anatuona tumesimama na mtu ambaye alihisi tuna mahusiano naye ya kimapenzi.
Mimi nilizingatia vyote hivyo kwa kipindi chote, nakumbuka sikuwahi kufanya mapenzi miaka minne. Kazi iliendelea vizuri mpaka mwajiri akanikabidhi biashara niisimamie mpaka kumlipa yule mwenzangu. Nilitengeneza pesa ya kutosha kipindi hicho. Lakini mwenzangu alikaidi na kuanza kujifunza kutumia vilevi .Alirudi usiku wa manane alipoamua yeye. Akanifanyia figisu mpaka nikafukuzwa kazi.
Nikaanzishisha biashara inayofanana na ya mwajiri wetu karibu. Ambayo ndiyo inaniingizia kipato mpaka leo. Ilinisaidia nikapata chuo na kujisomesha mwenyewe. Yule kijana baada ya miezi michache naye akafukuzwa kazi, biashara ikafa moja kwa moja. Akaja kwangu kuazima mtaji wa shilingi 60,000 japo pia alinidhulumu mpaka leo hatujaonana na hapatikani kwenye simu.
Nilijifunza mengi katika kuajiriwa,ukiwa jeuri na mkaidi huwezi kujifunza . Kuajiriwa kunatengeneza mazingira mazuri ya kufahamiana na watu, watakupenda hata kujitolea kukusaidia utakapo patwa na shida.
Bado natamani kuajiriwa japo nimejiajiri ili Kuongeza kipato zaidi. Nahitimisha kwa kusisitiza kwamba , huwezi kufanikiwa vizuri kujiajiri kama hujawahi kuajiriwa. Naomba maoni na ushauri pia , mawasiliano ni kupitia utotolemoja@gmail.com.

Upvote
2