Rodgers Bethody
New Member
- Sep 11, 2021
- 2
- 2
Moja kati ya changamoto inayowasumbua wajasiliamari chipukizi ni kushindwa kutambua kutambua namna bora ya kukuza biashara/kampuni zao na kuwa zenye mafanikio makubwa.
Wengi wao hushindwa kujifunza na kuelewa mchakato mzima ambao ndio nguzo muhimu ya kuendesha kampuni changa kuelekea kwenye biashara/kampuni zenye mafanikio.
Hivyo basi wameamua kuupokea kwa mikono miwili udhaifu huu wakati wakiwa na sababu lukuki za kushindwa kutafuta suluhu ya changamoto hii.
USA na Israel (kwa mfano) kwa muda sasa walifahamu wengi was wajasiliamali chipukizi wanaubunifu wenye tija lakini wengi wao hukosa mbinu/namna sahihi za kuwezesha kujenga biashara/kampuni kubwa(moja ya ujuzi mgumu Zaidi kuupata).
Venture capital ambao ndio hufadhili wajasiliamari chipukizi (startup) hutoa rasilimali viwezeshi kama Training,mentors and even provide skilled managers ambao jukumu lao kubwa ni kuleta mchakato wa namna bora kiuendeshaji pamoja na ukuaji katika ongezeko la thamani ya kampuni/biashara husika.
Ukifuatilia Podcast za makampuni kama Google,facebook,Ebay na starbucks utaweza kuona namna ambavyo wajasiliamari hawa waliweza kuunda timu na watendaji wenye weledi (skilled Excutive) katika kusaidia kukuza na kuwa hivyo zilivyo leo.
Kama unaendesha biashara/kampuni na umeanguka katika kundi hili(those who started without prior institute knowledge) makala hii inaweza kukufaa sana.
Hii yawezakuwa sababu tosha ya biashara/kampuni nyingi hususani Tanzania na Afrika kwa ujumla kushindwa kuyafikia malengo yao hata kama kuna uhitaji mkubwa wa huduma wanayotoa katika jamii inayowazunguka.
NI MUHIMU KUWA NA TIMU:
timu hii ni mkusanyiko wa watu wenye weledi na uzoefu wanaoungana katika kutimiza lengo moja.kufanya kila kitu peke yako hupunguza ufanisi katika lengo kusudiwa.
NI MUHIMU KUJIFUNZA UONGOZI:
kama kiongozi jukumu lako ni kusimamia mfumo na kubainisha udhaifu kabla udhaifu hauja athiri mfumo wenyewe.
Kila biashara kubwa au ndogo ni muhimu kuwa na mfumo. Mfumo husaidia utekelezaji wa majukumu ya kila siku kadiri mfumo unavyokuwa bora ndivyo ambavyo hupunguza utegemezi katika watu.
Hivyo basi sio suala la kukusanya watu wenye weledi pekee mpaka pale utakapoelewa sayansi ya mpangilio wa taasisi na uongozi madhubuti katika ukuaji wa biashara/kampuni husika.
VIPI UTAWEZA KUWAUNGANISHA UNAOWAHITAJI?
Watu sahihi kwenye timu yako unaweza kuwapata kwa njia zifuatazo
Kama sehemu ya bodi ya washauri;
Njia hii ni bora zaidi kwa wajasiliamari chipukizi maana haina gharama tofauti na njia nyingine.
Kuwapatia sehemu ya hisa katika kampuni;
Ni njia nzuri maana huwapatia sehemu ya umiliki wa kampuni hivyo hufanya kazi kwa weledi na kutumia muda mwingi katika KaZi za kampuni.
Kuwapatia gawio la kutoka kwenye faida ya kampuni;
Watu hawa huwa na uzoefu wa kutosha katika kujenga mfumo sahihi hususani katika usimamizi wa masuala ya kifedha.
Mfano halisi ni moja ya kampuni inayojishughulisha na shughuli Za mawasiliano nchini Botswana katika siku za mwanzo za uchanga wao ilikuwa ikiwaalika watendaji wastaafu waliohudumu kwenye kampuni kongwe kutoka USA waliokuwa wakifanya shughuli kama hizo pia.
"One thing that helped me was inviting retired executive to either come and talk to me or even spend some times with us .. You will not find people who are still working willing to do this and its not reasonable to ask them". Alisema mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo.
Pia mbinu hii nimeona ikitumika na kampuni kubwa ya nishati mbadala (Tropical Power) nchini Kenya wao hufanya KaZi na wakurugenZi wastaafu kutoka nchini German.
Iliwalazimu kulipia huduma kwenye umoja wa wakurugenzi wastaafu aliekuja kukaa nao kwa muda wa miezi sita nchini Kenya.
Alishirikiana na kampuni katika kila idara pia aliendesha coaching session katika kampuni hiyo.
"I would say in those six months he added 10 years to our development. By the time he left we had a system and had added German efficiency to our approach. Things like time management and planning were drilled into us like solders" alisema Mr. Mike Nolan C.O.O wa Tropical power.
Ni vigumu kutatua tatizo ambalo hujalitambua.waswahili tuna msemo usemao "kulifahamu tatizo ni nusu ya kupata suluhu yake".
Hivyo basi ni muhimu kujifunza kwa watu wenye weledi katika matatizo au changamoto zetu kuliko kudhania tunaweza kila kitu peke yetu
Siku hizi program za mafundisho mbalimbali zinapatikana kwa njia rahisi kupitia simu janja.
Dhumuni la makala hii ni kuwapatia mwanga na namna bora ya kuwaza katika mtazamo tofauti katika kufikia malengo yetu.
Asanteni

Upvote
1