Huwezi ukawa mzalendo mwenye akili timamu ukasema kuwa Magufuli alikuwa si kiongozi bora

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
John Pombe Magufuli ni rais ambaye amesifiwa sana ndani na nje ya nchi kutokana na sera zake za Tanzania kwanza, hapa kazi tu, kupiga vita rushwa, kubana matumizi, kujitegemea, kuziba mianya ya ufujaji pesa, na kuwekeza kwenye miundombinu ya viwanja, barabara, viwanja vya ndege, stand za mabasi, umeme, maji, madaraja, etc.

Kwa upande mwingine, JPM ni rais anayetukanwa sana hususani na watu ambao wanahisi hakuwatendea haki wakati wa utawala wake. Watu hao ni pamoja na wala rushwa, wazembe kazini, wezi wa rasilimali za nchi, majambazi, panya road, vyeti feki, wafanyakazi hewa, wafanya biashara za maji (kwenye magari), wasambazaji wa majenereta. Watu hawa hadi kesho watakuwa na mtazamo hasi, makasiriko hadi siku zao za mwisho.

Niwaombe tu wamtue JPM mioyoni mwao. Kusamehe kupo, basi haina budi kumsamehe pale ambapo unaona hamkutendewa sawa na matakwa yenu, ila alifanya kwa niaba ya Mama Tanzania.
 
..kilichomfanya atumie madaraka yake vibaya dhidi ya wapinzani ni nini?

..Magufuli alikuwa na malengo mazuri, tatizo lake alikuwa na tabia za kinyama na kikatili.
Sasa TABIA za kikatili maybe zilikuwa damuni,

Anyway, hivi mkandarasi anayekula pesa za wananchi na hajengi Barbara, unamchekea Ili iweje,

Mazuri na malengo mema ndio hayo tunayoyakumbuka kwake.

Upinzani wa kupinga Kila kitu pia ni WA kishamba, usingetufikisha popote,

Ule upinzani wa kamanda uchwara wa kubadili GIA angani!
 
..alitakiwa kufuata SHERIA.

..mtu asiyefuata sheria ni mhalifu.

..kuhusu wapinzani alitakiwa awashughulikie kwa kuwa na HOJA nzuri zaidi yao, na sio kutumia vyombo vya dola, na mahakama, kuwatesa, na kuwashambulia.

..damage aliyotuachia ktk vyombo vya dola, na mahakama, itachukua miongo kadhaa kuirekebisha.

..Tumefika mahali mahakama zetu haziwezi tena kutenda haki kwa wapinzani. Hiyo ni sehemu ya legacy ya Uraisi wa Magufuli.
 
Kukumbuka mabaya ya marehemu ukayafanya legacy ni Roho mbaya hiyo,

Hiyo ni kuhukumu bara letu la Afrika.
 
..mwenye roho mbaya ni huyo marehemu wenu.

..maisha ya mwanadamu ni kama kitabu.

..Mazuri na mabaya yanabaki kuwa kumbukumbu ya maisha ya mhusika.
 
Haina shida,

Tunza mabaya ya Magu yakuongezee pressure.

Sisi tunachukua mema yake, mabaya tunayaepuka.

Uamuzi ni wako.
 
..unaruhusiwa kujisahaulisha maovu yake kama namna ya ku cope na maisha.
 
Ila huwezi kumpamba akapambika, huwezi msifu akasifika, huwezi kumchukia akachuchika.

Yule alikuwa chunvi kwenye mboga ila tatizo ilizidi mpaka ikawa hailiki.
 
..unaruhusiwa kujisahaulisha maovu yake kama namna ya ku cope na maisha.
Nimekwambia nimechagua upande wa mema na HAKI,

Ndio maana tupo pamoja kudai Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote Ili kufikia ndoto ya Magu juu ya Tanzania mpya Kwa njia Bora zaidi.

Lakini uzalendo wa mtu yule juu ya wananchi maskini Si wa kutiliwa shaka.
 
..Ni wa kutilia mashaka kutokana na matendo ya ukatili wakati wa uongozi wake.

..kiongozi anayenajisi mahakama na vyombo vya dola anakuwaje mzalendo?
 
Kamwe haitotokea na haiwezekani tena nchi hii kubadirishwa na kiongozi yeyote yule kama hatujabadiri Katiba na baadhi ya sheria zetu

Nchi ambayo sheria haziwi chochote kwa mafisadi..?

Ulitegemea nini JPM afanye dhidi ya watu kama hao, ni wapi ambako hakukuwa na usiganwaji wa katiba na sheria ambako mwananchi wa kawaida angeweza kusikilizwa na kupewa haki yake?

Si mahakama wala bunge ambako mwananchi angesikilizwa na kupatiwa haki zake

Kwa kiongozi yeyote hata sasa akipatikana, ambaye ni mzalendo kama Magufuli, mpenda haki na asifanye kama alivyokuwa akifanya JPM kuinusuru nchi hii

Sector zote zimeoza, na kiongozi kama JPM anapotaka kunyoosha nchi, lazima watu waseme anaingilia mihimili mingine ilihali hata hiyo muhimili imeoza

Ieleweke, Mahakama na au bunge zinapoacha kutenda haki, zinasigina katiba, enzi hizo ilikuwa ni kawaida kwa mwenye fedha kumfunga mtu yeyote bila kosa

Kwa mambo hayo kama kiongozi mpenda haki, kwa nini usiwachomoe hao?
 
..alitakiwa kufuata SHERIA.

..mtu asiyefuata sheria ni mhalifu.

..kuhusu wapinzani alitakiwa awashughulikie kwa kuwa na HOJA nzuri zaidi yao, na sio kutumia vyombo vya dola, na mahakama, kuwatesa, na kuwashambulia.

..damage aliyotuachia ktk vyombo vya dola, na mahakama, itachukua miongo kadhaa kuirekebisha.

..Tumefika mahali mahakama zetu haziwezi tena kutenda haki kwa wapinzani. Hiyo ni sehemu ya legacy ya Uraisi wa Magufuli.
Wanaofuata Sheria wangewasaidia Nini? Kipi Cha maana wamekifanya?
Kutwa kucha hapa kulalamika mambo hayaendi Bado mnamlaumu Magu!
🤔
 
Kamwe haitotokea na haiwezekani tena nchi hii kubadirishwa na kiongozi yeyote yule kama hatujabadiri Katiba na baadhi ya sheria zetu

Nchi ambayo sheria haziwi chochote kwa mafisadi..?

Ulitegemea nini JPM afanye dhidi ya watu kama hao, ni wapi ambako hakukuwa na usiganwaji wa katiba na sheria ambako mwananchi wa kawaida angeweza kusikilizwa na kupewa haki yake?

Si mahakama wala bunge ambako mwananchi angesikilizwa na kupatiwa haki zake

Kwa kiongozi yeyote hata sasa akipatikana, ambaye ni mzalendo kama Magufuli, mpenda haki na asifanye kama alivyokuwa akifanya JPM kuinusuru nchi hii

Sector zote zimeoza, na kiongozi kama JPM anapotaka kunyoosha nchi, lazima watu waseme anaingilia mihimili mingine ilihali hata hiyo muhimili imeoza

Ieleweke, Mahakama na au bunge zinapoacha kutenda haki, zinasigina katiba, enzi hizo ilikuwa ni kawaida kwa mwenye fedha kumfunga mtu yeyote bila kosa

Kwa mambo hayo kama kiongozi mpenda haki, kwa nini usiwachomoe hao?

..magufuli hakuwa kiongozi anayependa haki,wala sheria.

..katika utawala wake alihakikisha bunge halina nguvu, na aliitumia mahakama kisiasa.
 
Back
Top Bottom