Huyu angekuwa mlinzi wako ungefanyaje?

Huyu angekuwa mlinzi wako ungefanyaje?

Kashaija

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2008
Posts
255
Reaction score
62
Jamaa yangu mmoja anaye mlinzi wa usiku nyumbani kwake, kawaida ya huyu mlinzi huwa anaingia kazini saa moja jioni anatoka saa kuminambili asubuhi ila huwa ana kawaida ya kulala na kusinzia wakati yuko lindoni.

Siku moja tajiri yake alikuwa amepanga safari ambayo angesafiri kesho yake alfajiri sana. Siku hiyo alipoamka na tayari akiwa ameshajiandaa kwa kila kitu akataka amuage Mlinzi wake kwamba hatakuwepo kwa takribani wiki nzima, hivyo kumtaka awe makini na ulinzi.

Hapo hapo Mlinzi akamwambia kwamba usiku wa leo nimeota unasafiri safari ya mikoani na basi likapata ajali na kuua watu wengi ikiwa ni pamoja na wewe, hivyo ningekushauri uhairishe safari yako hata uende kesho. Tajiri kwa shingo upande na baada ya kutafakari sana akaamua kuahirisha safari, na kesho yake akapata habari kwamba gari hilo hilo ambalo angesafiri nalo limepata ajari na kuua watu wengi. Alimshukuru sana mlinzi wake kwa kuokoa maisha yake.

Baada ya siku kadhaa, Mlinzi huyo akiwa amelala, vibaka/wezi wakavunja na kuiba vitu vingi ndani. Kesho yake Tajiri alikasirika sana na kumfukuza kazi kwamba analala usingizi badala ya kulinda, lakini akasahau kwamba usingizi huo huo uliokoa maisha yake.

Swali, je ungekuwa wewe ndo tajiri huyo ungefanyaje? Kipi bora, maisha au mali?
 
...Mimi ningeangalia mali zangu kwani siwezi kutegemea bahati nasibu ya usingizi wa mlinzi awe mtabiri wa maisha yangu kwani yeye pia ni binadamu na sitaki kuamini kuwa ana uwezo wa kujua kuwa kesho kutanitokea nini? Huenda siku hiyo ilikuwa amebahatisha tu hiyo basi kupata ajali. Mbona hakuota kama wezi watakuja kuvunja na kuiba aniambie at least tuongeze ulinzi au tuweke mtego tuwakamate hao wevi??
 
Back
Top Bottom