Nyumba ni ya familia na wanaishi pamoja na wapangaji. Binti kamaliza elimu yake ya juu na kufanikiwa kupata kazi, ili aweze kuwa huru kaamua kuhama nyumbani na kutafuta nyumba ya kupanga. Baba yake kamwambia badala ya kwenda kumpa pesa ya kodi mtu mwingine ni bora abaki palepale nyumbani, ila kile chumba anachoishi akilipie na mahitaji mengine ajitegemee kama vile chakula n.k. Baba anadai hawezi kuacha binti yake akampe mtu mwingine kodi ya nyumba wakati yeye ndie kamsomesha. Binti anaishi kwao kama mpangaji mwingine tu...
Hivi wakuu hii imekaaje?? Inakubalika??
sawa lakini kuna uhuru fulani ambao binti atakosa...... Lakini kali kuliko ni pale ambapo binti anaishi kama wapangaji wengine tu....hii haijatulia.Kwa upande mwingine sio vibaya...kama kuna chumba ambacho mpangaji yeyote angekaa, why not binti yake??

Mwisho atamwambia kuliko kwenda kumfaidisha mwanaume mwingine ni bora amuoe yeye,maana ye ndie kamsomesha.

Sijajua uhuru tunouzungumzia hapa ni wa vipi!

Lakini nijuavyo mimi ni kuwa ishu si baba kupata senti za upangaji tu!

Binti kwenda mbali kujitegemea ni zaidi ya kodi!

Actually kuwa mbali na nyumbani inamwezesha mtu ku'interact na jamii kwa mapana zaidi! Kuna kero za upangaji ambazo tuliopata kupanga wote tunazifahamu, ambapo kwa kukaa nyumbani atazisikia redioni!, na kwa hali hiyo binti hatajengeka ipasavyo!

Kuna watu watakuwa Limited kufika pale nyumbani kwake, kisa ni kwa baba-mtu...hata kama anaishi kwa kupanga watu hawatajua hilo, watajua anaishi chini ya wazazi, hivyo umakini fulani unahitajika kuingia nyumbani kwake!

Hivyo kumshauri binti apange kwa babaye ni kosa kubwa, aidha ni kuvuruga saikolojia ya binti...Huyu mzee atakujaona vituko ambavyo hakutarajia, na atapata presha bure!