Gnyaisa
Member
- Jul 13, 2021
- 23
- 24
“Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli, iwafae maishani.”
Wahenga tutakuwa tunaukumbuka huu ubeti wa shairi maarufu sana enzi tunasoma shule ya msingi. Katika utenzi huo tunaambiwa huyu baba alikuwa anatoka safari ya mbali sana na mapaja yake yote yalikuwa yamevimba huku mwili ukitetemeka. Kwa namna watoto wake walivyomuona walijua “mshua” si wa kupona hivyo haraka wakataka awagawanishe chochote. Mzee akaamua kuwarithisha BUSARA.
Kuna maswali kadhaa tunapaswa kujiuliza kama watu wazima; Mzee alienda wapi? Hii safari ya mbali kiasi cha kurejea tu nyumbani anakutwa na mauti ikoje? Watoto wake walifuata maelezo yote ya wosia wakatajirika, kwanini watoto wa Kitanzania bado ni mafukara licha ya kuusikiliza wosia wa baba huyu tangu tukiwa shule za msingi? Zaidi ya asilimia sabini na tano (75%) ya Watanzania ni wakulima, kwanini asilimia hiyohiyo sabini na tano ndo maskini wa kipato?
Tukitazama jiografia ya mataifa sita yanayounda jumuiya ya Afrika Mashariki, taifa la Tanzania lina bahati ya pekee ya kuwa na hali ya hewa nzuri na ardhi yenye rutuba tele kuweza kulima kila aina ya zao. Tanzania ni taifa pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati lenye eneo kubwa lisilotumika kwa shughuli zozote za uzalishaji. Zaidi ya asilimia 60 ya ardhi yote ya Tanzania ni maji ya mito na maziwa, hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Tanzania ina jumla ya hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, ni hekta 331,490 pekee ndizo zilizowekewa miundombinu muhimu ya umwagiliaji ambapo pia uzalishaji wa hekta hizo ni wa kusuasua licha ya kuwa na miundombinu hiyo.
Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki inayoundwa na mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya, Sudan Kusini na Tanzania inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 180. Mtaji huu mkubwa wa watu ni fursa ya kipekee kwa wakulima wa Kitanzania ambayo hata hivyo tumeiacha ipotee bure.
Wakati mataifa wanachama wa jumuiya hii yakikumbwa na ukame wa mara kwa mara unaopelekea upungufu wa chakula katika nchi zao, kwa upande wa Tanzania tuna uhakika wa maji ya kutosha na ardhi yenye rutuba lakini tumeshindwa kuzalisha na kukidhi mahitaji ya soko.
Tanzania bara inaundwa na kanda tano zenye zaidi ya mikoa 25 ambapo kila kanda ina fursa ya kipekee ya kilimo tofauti na kanda nyingine. Kuna kanda ya Nyanda za juu Kusini inayoundwa na mikoa ya Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma. Hii ni mikoa inayoilisha Tanzania kwa chakula kutokana na mvua za kutosha na ardhi nzuri inayofaa kwa kila aina ya zao. Maziwa makuu ya Nyasa, na Rukwa yako katika ukanda huu. Mabonde makubwa pamoja na mito kadhaa isiyokauka inapatikana katika kanda hii. Hata hivyo, hatujafanikiwa kabisa kuzitumia fursa hizi ipasavyo.
Kuna kanda ya kati inayoundwa na mikoa ya Dodoma, Kigoma, Singida naTabora. Tunayo pia kanda ya ziwa inayoundwa na mikoa ya Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu. Tuna kanda ya kaskazini inayoundwa na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga na tuna kanda ya Pwani inayoundwa na mikoa ya Dar es salaam, Lindi, Morogoro na Mtwara.
Kanda zote hizi zina ardhi yenye rutuba na maji ya kutosha ya mito, maziwa na yale yanayopatikana ardhini, mbona wosia wa huyu baba haujazaa matunda kama ulivyozaa kwa watoto wake?
Nadhani kuna umuhimu wa kurudi shule ya msingi na kutafakari juu ya swali la wapi alienda huyu baba. Pengine tukiijua hii safari yake ya mbali tutajua namna bora ya kutajirika kupitia kilimo. Baba hakuwa na pumzi za kutosha kutuambia aliona nini huko nchi za mbali. Pengine aliona wenzetu wakitumia matrekta ya kisasa na teknolojia bora za umwagiliaji na si jembe la mikono na kilimo cha mvua tunachotumia sisi. Pengine aliona njia bora za usindikaji mazao na uongezwaji thamani na sio njia za maghala tunazotumia sahizi.
TUMTAFAKARI BABA.

Upvote
0