KERO Huyu babu wa radio Free Africa ana tofauti gani na kiboko ya wachawi? na je kwanini hafungiwi?

KERO Huyu babu wa radio Free Africa ana tofauti gani na kiboko ya wachawi? na je kwanini hafungiwi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mfate42

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
4,034
Reaction score
4,792
Habari za muda huu ndugu wana JamiiForums,

Naomba kuuliza hivi huyu mzee anaejiita babu, ambae anarusha matangazo yake ya uganga wa kienyeji kupitia kituo Cha Radio Free Africa, Mwanza ana tofauti gani na yule aliyefungiwa kule Buza, anayejiita kiboko ya wachawi.

Nimejaribu kusikiliza kwa umakini kabisa, naona kabisa ni utapeli tu. Hata wanaopiga simu kutoa ushuhuda nao ni Kama vile wamepangwa ili wawaaminishe watu kwamba huyu babu ni mganga haswa.

Serikali ikalitazame hili, yasije yakawa ya Makenzie wa Kenya.
 
Back
Top Bottom