Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Twende moja kwa moja kwenye kisa. Rafiki yangu kaniomba ushauri kuhusu huyu bidada.
Huyu rafiki alikodi fremu maeneo yaliyochangamka karibu na soko kwa ajili ya kupika na kuuza supu. Wateja wa huyu rafiki wakaanza kulalamika kuwa wanauziwaje supu bila chapati mbili? Akaona ni bora amsake bidada walau awe anapikia pale chapati na kuwauzia wateja lakini faida ni yake mwenyewe, hatozwi hata mia na huyu rafiki yangu.
Mauzo ya supu yalikuwa yakienda kama kawaida nyakati zote, asubuhi, mchana, jioni hata usiku. Siku chache baadae, bidada alianza kupika na chai au maziwa nyakati za asubuhi, baada ya kama siku tatu akaanza kupika ugali na mbogamboga nyingine na kuuzia ndani ya hiyo fremu.
Shida ikaanzia pale wateja walipoanza kuisusa supu! Mi nilikuwa mmoja wao, nikaona sasa ninywe supu ya 1,500 na ndimu kama kifungua kinywa halafu niache chai yangu ya maziwa ya 300 na chapati 4 za 300 300 nikashiba, inaingia akilini kweli?
Hali ilikuwa siyo kwangu tu hata na wateja wengine nyakati za mchana! Ikafikia hatua supu inalazwa, au kumwagwa! Process zote hizi hazikuwa shirikishi kwa rafiki yangu, yaani hakushirikishwa!
Sasa ni siku ya tatu tokea binti aongeze ubunifu mwingine wa kupika supu ya kuku na pweza wakati rafiki yangu ni mpishi wa utumbo wa mbuzi na ng'ombe [emoji23] Biashara imebuma [emoji24]
Ndo ananiomba ushauri amfanyeje huyu bidada? Hata hiyo kauli ya kwenye title sio ya kwangu, ni ya huyuhuyu rafiki yangu!
Istoshe binti kazungumza na mwenye fremu kuwa baada ya miezi mitatu ya jamaa kuisha, ataongeza pesa kwenye kodi ya maelewano ili fremu apewe yeye!
Nawasilisha, ushauri tafadhari!