Huyu Comedian wa Kawe Media fm alikuwa anatania tu au alimaanisha?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Eti " Watu wote wanaomiliki Gari aina za Vitz na IST wasijihesabie kuwa wanamiliki Magari bali waseme tu kwamba wanamiliki Majenereta yanayotembea kwani kwa Mwanaume aliye na akili timamu na mwenye Pesa hawezi kumiliki Gari dogo ila atamiliki Gari kubwa ili kuonyesha Uanamume wake ".

Kwa usalama wake kutoka kwa wenye hayo Magari Majenereta sitoweza kumtaja jina hapa ila kama Wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Kawe Media fm ( siyo jina lake halisi ) jirani kabisa na Msasani Club Kawe utakuwa umeshamjua huyo Comedian.

Haya wenye hayo Magari Majenereta Vitz na IST hebu jitokezeni mtiririke na mserereke juu ya kauli hii je mnadhani alikuwa tu anatania au amemaanisha?

Nawasilisha.
 
Wewe unadhani alikuwa anatania tu au katupa jiwe gizani / kamaanisha kiukweli ukweli?

Ni kweli hizo gari kwa mwanaume hazifai kutokana na mauomba ya wanaume kuwa makubwa kuliko wanawake pia urefu.
Ila tatizo linakuja kwenye hela ya ziada ya kununua hayo magari makubwa....
Ujue wengi wenye hizo baby walker wengi wao wamekopa sasa mtu kukopa zaidi ya 20mil ili akanunua usafiri anaona ajikune pale anapoweza
 

Tanzania ya vi wonder.
 

Mkuu mbona na Wewe haya maelezo yako yaliyojaa utetezi fulani hivi yanaonyesha kama vile pia unamiliki Gari Jenereta Vitz au IST? Kuwa mkweli na muwazi tu Mkuu kuliko kuzunguka zunguka utadhani Refarii wa mechi ya Simba na Yanga Israel Mujuni Nkongo.
 
Kuna mtu alisema.." Sijui njia ya kufikia mafanikio ila njia moja yenye uhakika ya kufeli ni kujaribu kumfurahisha kila mtu".
 
Vipi Mkuu mbona umeandika kwa hisia kali sana au na Wewe mwenzetu labda unamiliki Gari Jenereta kati ya Vitz au IST?
Sijawahi kumiliki gari ya aina hiyo. Gari yangu ilikuwa na cc 3000 lakini nilichogundua ni kuwa mwenye Vitz anafurahia zaidi maisha kwa kuwa anaweza kwenda umbali mrefu kwa ghrama nafuu sana. Sasa nataka kuiuza na mie nihamie kwenye Vitz maana uchumi unabana sana...
 
Mkuu mbona na Wewe haya maelezo yako yaliyojaa utetezi fulani hivi yanaonyesha kama vile pia unamiliki Gari Jenereta Vitz au IST? Kuwa mkweli na muwazi tu Mkuu kuliko kuzunguka zunguka utadhani Refarii wa mechi ya Simba na Yanga Israel Mujuni Nkongo.

Toka nimezaliwa sijawahi endesha VITS/IST.....
Nimepanda IST mara 1 Arusha, VITS nimepanda siku 1
Gari niliyo nayo ni SUV ya kawaida ila uzuri yenyewe haiko kwenye upande wa taxi
 
Ukikaa kumsikiliza sana kila mtu hapa Duniani hutofurahia maisha.
Kuna aina mbili za watu wa kutowasikiliza sana. Wale walioshindwa sana na wale waliofanikiwa sana. Hawa ukiwafuatilia, wataishia kukuchanganya ubongo...
[emoji106]

-Ndumilakuwili-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…