Huyu dada, hawezi kunipa limbwata kweli?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wakuu habari?

Mnavyojua tena, wanaume tumeumbwa kutamani na kupenda; hivi karibuni niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja anafanya biashara ya kununua madini mkoa mmojawapo huko kanda ya ziwa.

Huyo dada nilimpenda kutokana na uchangamfu wake, na uhusiano wetu ulianzia club moja, nilipoenda kupumzisha akili. Ndipo nilipomuona, na kumpatia namba yangu ili aweze kunitafuta. Na kweli alinitafuta, na mahusiano yakawa moto moto.

Mnavyojua tena, mimi huwa napenda kujifunza vitu kupitia watu mbalimbali; nikajaribu kumdadisi namna anavyofanya hiyo biashara, ili ikiwezekana na mimi huko mbeleni niweze kuifanya.

Katika majadiliano, ikaonekana huwa anajihusisha mara kwa mara na mambo ya uganga katika kujikinga na maadui mbalimbali katika hiyo biashara. Yaani yeye kwenda kwa mganga, ni sawa na muumini aliyeshika dini yake anavyoenda kusali siku ya jumapili au ijumaa.

Akiona mdudu yeyote, lazima awasiliane na mtaalamu wake ili kujua kama kuna usalama ama vipi.

Kinachonipa wasi wasi zaidi, jana tulikesha naye maeneo fulani ya mapumziko, akaniambia ana safari leo ya kwenda sehemu, lakini hiyo sehemu anayotaka kwenda inautata, na hawi muazi kuniambia anaenda kufanya nini.

Mbaya zaidi, alikuwa safari ya kama mwezi hivi, ambapo mawasiliano mimi naye yalikuwa yanasua sua hasa kwa upande wangu, nilikuwa simtafuti mara kwa mara.

Kutokumtafuta ikawa ni sehemu ya ajenda; kwa nini nilikuwa nafanya hivyo, au kuna mchepuko mwingine? Nikajaribu kujitetea hapa na pale, lakini likawa limeisha kwa shingo upande.

Hofu yangu; hii safari ambayo ameenda leo, inawezekana anaenda kushughulikia biashara zake, lakini na wasi wasi pia, anaweza kunipiga limbwata nikawa sina jeuri kwake.

Wakuu, nifanyeje ili nikimbie hichi kifungo kinachokuja mbele yangu?
 
Acoding to bible inasema " 𝐢𝐧𝐚𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐮𝐬𝐢𝐦𝐮𝐚𝐜𝐡𝐞 𝐦𝐰𝐚𝐧𝐚𝐦𝐤𝐞 𝐦𝐜𝐡𝐚𝐰𝐢 𝐤𝐮𝐢𝐬𝐡𝐢,,

𝐧𝐚 𝐦𝐭𝐮 𝐲𝐞𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐚𝐧𝐚𝐲𝐞𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐠𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐜𝐡𝐚𝐰𝐢 𝐩𝐢𝐚,
wewe endelea kucheka cheka naye
 
Mimi namshauri huyo dada akupige tu limbwata..hata la buku 5 tu akili yako ikae sawa..maana unahangaika si mchezo
Tatizo mnatushawishi sana, na hayo mambo yenu
 
Acoding to bible inasema " 𝐢𝐧𝐚𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐮𝐬𝐢𝐦𝐮𝐚𝐜𝐡𝐞 𝐦𝐰𝐚𝐧𝐚𝐦𝐤𝐞 𝐦𝐜𝐡𝐚𝐰𝐢 𝐤𝐮𝐢𝐬𝐡𝐢,,

𝐧𝐚 𝐦𝐭𝐮 𝐲𝐞𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐚𝐧𝐚𝐲𝐞𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐠𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐜𝐡𝐚𝐰𝐢 𝐩𝐢𝐚,
wewe endelea kucheka cheka naye
Mkuu, nifanyeje ili niwe naye mbali?
 
Wakuu habari?

Mnavyojua tena, wanaume tumeumbwa kutamani na kupenda; hivi karibuni niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja anafanya biashara ya kununua madini mkoa mmojawapo huko kanda ya ziwa.

Huyo dada nilimpenda kutokana na uchangamfu wake, na uhusiano wetu ulianzia club moja, nilipoenda kupumzisha akili. Ndipo nilipomuona, na kumpatia namba yangu ili aweze kunitafuta. Na kweli alinitafuta, na mahusiano yakawa moto moto.

Mnavyojua tena, mimi huwa napenda kujifunza vitu kupitia watu mbalimbali; nikajaribu kumdadisi namna anavyofanya hiyo biashara, ili ikiwezekana na mimi huko mbeleni niweze kuifanya.

Katika majadiliano, ikaonekana huwa anajihusisha mara kwa mara na mambo ya uganga katika kujikinga na maadui mbalimbali katika hiyo biashara. Yaani yeye kwenda kwa mganga, ni sawa na muumini aliyeshika dini yake anavyoenda kusali siku ya jumapili au ijumaa.

Akiona mdudu yeyote, lazima awasiliane na mtaalamu wake ili kujua kama kuna usalama ama vipi.

Kinachonipa wasi wasi zaidi, jana tulikesha naye maeneo fulani ya mapumziko, akaniambia ana safari leo ya kwenda sehemu, lakini hiyo sehemu anayotaka kwenda inautata, na hawi muazi kuniambia anaenda kufanya nini.

Mbaya zaidi, alikuwa safari ya kama mwezi hivi, ambapo mawasiliano mimi naye yalikuwa yanasua sua hasa kwa upande wangu, nilikuwa simtafuti mara kwa mara.

Kutokumtafuta ikawa ni sehemu ya ajenda; kwa nini nilikuwa nafanya hivyo, au kuna mchepuko mwingine? Nikajaribu kujitetea hapa na pale, lakini likawa limeisha kwa shingo upande.

Hofu yangu; hii safari ambayo ameenda leo, inawezekana anaenda kushughulikia biashara zake, lakini na wasi wasi pia, anaweza kunipiga limbwata nikawa sina jeuri kwake.

Wakuu, nifanyeje ili nikimbie hichi kifungo kinachokuja mbele yangu?
Dah! Tunaenda kumpoteza comrade.
Hata kama anaenda kwa zile shughuli za giza lazma akuangalie na nyota yako boss
 
Back
Top Bottom