Huyu dada natumai atakuwa mke wangu peponi

Huyu dada natumai atakuwa mke wangu peponi

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Tuna dada yetu mmoja, mtoto wa shangazi ambaye ni mkubwa sana kuliko mimi na hata amewahi kunilea udogoni kwangu. Huyu dada kwa kweli alikuwa ni mzuri sana na mwenye mapozi safi sana ya kimaumbile.

Ikitokea kishindo mtaani wala hashtuki na kufazaika kiasi cha kupoteza muonekano wake.

Akifurahi hata jambo gani wala hacheki kwa sauti kubwa kila mmoja akamsikia, bali hukenua tu na kuufanya uso wake uzidi kung'ara.

Akitembea huwa anatikisika bila kujilazimisha.

Sote pale mtaani tulijua hivyo kuwa tuna dada mzuri sana.Bahati mbaya sana aliolewa bila ridhaa yake na mwanamume mmoja mbaya sana wa sura na tabia na sisi sote tukawa hatukupendezewa na hilo.

Baada ya kuzaa naye watoto kadhaa akaachwa. Haikuchukua muda akatokea mume mwengine si mbaya wa sura kama yule wa mwanzo lakini ni jitu rogi sana na mwenye tabia mbaya za kila aina.

Ulimwengu wa ndoto ni ulimwengu mwengine kabisa.Unaota maeneo ambayo hujawahi kufika, kufanya mambo ambayo yanafanana sana na ya kawaida lakini hujawahi kuyafanya kabisa na pengine huna mpango wa kuyafanya

Iko siku unaweza ukaota ndoto mbaya sana kiasi kwamba ukishtuka kutoka usingizini unaogopa hata kulala tena na unaweza ukaamsha wenzako au kutamani uhame chumba.

Na Iko siku unaweza ukaota ndoto nzuri sana lakini ikataika njiani pale ulipokuwa unatamani ufikie mwisho wake.

Unajaribu kulala tena ili imalizike lakini usingizi hata ukija tena ile ndoto haijirudiii.

Huyu dada yetu kwa sasa ni mzee kiasi na mgonjwa mgonjwa.Sura nayo tukiwaonesha watoto wetu na wenzetu vijiweni hawaamini kuwa alikuwa mzuri wa kumvutia kila mtu kijijini.

Cha ajabu ni kuwa katika wiki za hivi karibuni tumekuwa tuko karibu sana na anajijia mara kwa mara katika ndoto katika ile sura na uchangamfu wake wa ujanani kwake.Juzi moja tulikuwa tunaogelea kwenye maji na sikujua kuwa ilikuwa maji ya bahari au ya ziwani.

Mimi binafsi najua kuogelea lakini sidhani kuwa dada anaweza kuogelea tena katika mtindo kama ule.Tulikuwa tunaogelea tukiwa tumesimama ndani ya maji huku tukiwa tumekaribiiana na tunazungumza mambo fulani kwa upole sana.

Sehemu za chini, mguu wangu ukagusana na wake. Japo tulikuwa tumo ndani ya maji lakini mguu wake ukatoa joto lenye ladha nzuri sana. Kikawaida mimi huwa namuheshimu sana na kumuonea haya na kwa jinsi alivyowahi kunilea pale angenikemea kwanini mguu wangu nimeugusanisha namna ile. Cha kushangaza na yeye akazidi kujigandamiza na mimi bila kutetereka kwenye hadithi aliyokuwa akinisimulia.

Mara looh! nikashtuka huku nikiwa natamani niendelee kufurahi na dada yangu nione mwisho tungefikia wapi.
 
Back
Top Bottom