Huenda ana mtu ameshaahidiana nae kitambo hivyo upo kama plan B, au huenda ana ngoma anaogopa atakuambukiza ama utamshauri kupima hivyo akakukosa kimoja. Hebu mshauri mwende HIV Test akikubali basi jua wewe ni Plan B!
Shukrani mkuu,nitajaribu kumchomekea kuhusu swala zima la HIV na kama yuko tayari siku moja kwenda kupima na 'to be' wake,nione response yake!
Ni ngumu kutuelewa wanawake sometimes..... baadhi yetu tuna wivu wa ajabu hata kwa vile tusivyovitaka.....nakushauri tafuta muda zungumza nae kimoja,mwambie unataka kuelewa msimamo wake wa mwisho.....na heshimu maamuzi yake as in kile atakacho kisema.....akikataa mpotezee mazima,tulishapenda sana tusikopendwa bwana na maisha yakaendelea tu.....utakutana na mwingine jiweke kwanza huru kwa nafsi na kubali matokeo.....usiwe mtu wa kutegemea miujiza,unapoteza tu muda wako....yupo atakayekupenda hadi ujiulize alikuwa wapi....tulia!!
Shukrani Mkuu nimekuelewa vizuri na nitafanya kama ulivyonishauri
kila ukiona haumuelewi mwanamke basi ujue ndio unamuelewa. ongeza bidii kaka
Mkuu kloro nitakaza lakini this time is last,na akileta gozi basi sitamrudia tena!
mnh pole nahisi kakuweka pending,akikosa anayemtaka ndio akuchukue wewe....
hajakupenda sana upo kama second choice yake,solusheni na wewe usimpende kwa sana mweke second best na yeye...
penda unapopendwa kaka usiwe tayari kumuoa mtu anayekuchukulia kama second best kny choice zake!
tafuta mdada mwingine atakayekupenda wholy!
mwambie plan zako kuwa unatafuta msichana kwa sasa,na ukimpata mtambulishe yeye kama best friend wako...
huyu dada anakasirika na anakuwa na wivu kwa sababu anafeel threatened position yake kwako,ikiwa utamshirikisha ktk process nzima ya kutafuta galfriend kuanzia unamsaka mpk unampata itampelekea yeye ahisi kuwa involved,na hivyo kumfanya afeel secured na position yake kwako.....
lastly,hata hivyo viwanja mshirikishe muwe mnatoka wote watatu....trust me akiendelea kununa mpotezee!:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::mullet:
Asante dada,inawezekana kweli ananipenda tu kama kaka na anipendi kama mwanaume.Kama ulivyosema safari hii nitamchukulia kwa umakini sana na hata kama atanikubali,swala la kumuoa halitakuwa la mara moja.Na mimi nitamringia na nitamuweka kiporo kwanza!!
Kuhusu kumshirikisha kutafuta msichana mwingine au kutoka watatu naona haitasaidia sana.Huwa akinuna kama hivi na tusipowasiliana kwa muda mrefu kwani ni yeye ndiye huwa wakwanza kuniandikia jumbe tena ukizisoma katikati ya mistari waweza fikiri kuwa na mtu anamuandikia mpenzi wake.
Kifupi sitamshirikisha na nikikutana nae safari hii kisipoeleweka ndiyo itakuwa mwisho wa mimi na yeye na nitamwambia wazi kuwa sitaki kabisa niwe rafiki wala kaka yake na tusitafutane tena.
[/COLOR]
OOOOOH LOVE, LOVE, LOVE. Every one talks about it but none knows what is it.
Hiyo si kushauri kwa sababu mbili: Kwanza unaweza kupata jawabu usiyoipenda na baadaye siku za mbele ukaitumia hiyo kama reference. Pili si wote wako tayari kuzungumza uhusiano wao uliopita. Unaweza ukamuudhi.
Nikirudi kwenye mada kuu, pengine anaweza kuwa yuko "serious", anakupenda kama rafiki, kama kaka na anakasirika anapokuona na mwengine kwa sababu ya wivu kuwa kuna mtu anachukua nafasi yake. Labda muulize kwa nini hataki uhusiano na wewe lakini ananuna, "hakuruhusu" kuwa na uhusiano na mwengine.
Zungumzeni, ni kwa kuzungumza tu watu huelewana, na wala sio kumwonesha kuwa kama yeye hakutaki wengine wanakutaka.
Jambo ambalo ningekushauri usifanye ikiwa bado unamtaka, ni kuwacha hiyo tabia ya mademu wengine mpaka hapo utakapojua moja.
Kila la heri.
Nimekuelewa sana broda!
Mkuu muhubiri pole sana kwanza, najua mtihani unaopata na ndio jinsi mapenzi yalivyo. Itategemea na mda wako uliokuwa nao wa kusubiri mpaka upate jibu kamili utakalo ridhika nalo wewe. Mpaka sasa naona ujaridhika bado na jibu lake na kuna vitu vinakufanya ufikirie kuna siku utapata jibu ambalo unataka kulisikia.
Kipindi hiki chote mnachofahamiana hujawahi kumuona na mtu mwingine wala kumsikia akimtaja mtu mwingine kwenye mazungumzo yenu?
Kwa vile huwa mna flirt mara nyingi,je wakati mko pamoja mna flirt ushawahi kujaribu kuvuka mpaka kwa vitendo kumsikilizia reaction yake au kila saa umekua ukijaribu kumtongoza tu?
Kuwa na wivu hio sio tatizo , anaweza kuwa na wivu kwa vile anaona kuwa hutakuwa na mda wa kupoteza nae kumpa hio company anayotaka kutoka kwako.
Mkuu Wenger asante sana kwa mawazo yako.Kifupi huyu demu mcharuko yaani simuelewi kabisaa nini anachotaka kutoka kwangu manake hata huo urafiki na ukaka anaousema ni wa mdomoni tu lakini matendo yake hayafanani kabisaa.Nimeendelea kumfuatilia na kutegemea jibu zuri kwa sababu mwenyewe ananionyesha dalili hizo lakini majibu yake utata mtupu.
Kusema ukweli nikiwa naye hasa club huwa namshika sana,isipokuwa hajawahi kunirihusu kula mate japo nimejitahidi sana kumshawishi.Binafsi sijawahi kumuona na mtu mwingine na tunaishi mbalimbali kidogo.Kipindi chote nachowasiliana nae huwa nikitaka kukutana naye,sipati shida.Nampigia au namuandikia na siku nitayopanga(mara nyingi weekend) huwa aikatai.Isipokuwa sijui schedule yake ilikuwaje kipindi chote tulipokuwa hatuwasiliani.
Kuhusu swala la wivu,inawezekana uko sawa hapo.
Act like a man. Stop clinging on her. Two years and you're still hitting on her? Move on bro. Be a man. Another piece if advise: kama mpaka sasa hivi hujamwelewa, then hutamwelewa hata kama ikimwoa. Move on man.
Its not easy as u suggest mkuu hayajakukuta haya labda!!
Mhubiri wewe ndio haueleweki ukimfukuzia huyu dada unaendelea kutoka na wengine,ni vigumu yeye kukuamini hebu tulia kwake kwa muda atakuamini na kukukubali.Anakasirika kwakuwa anakupenda hilo hawezi kuigiza.
Mkuu;je wewe unaweza kukaa aka mbili unafukuzia demu,hakupi na ukaendelea tu bila kutafuta kwingine uchakachue?
Wewe kuwa king'ang'anizi wa kumuomba uhusiano nae mpaka kieleweke,muambie kitaani na marafiki zako wote wanajua ya kuwa nyie ni wapenzi hivyo basi hakuna atakayekubali ya kwamba ndani ya miaka mi2 hujamtenda.
shukrani mazee,nitakomaa nae kibingwa lakini kwa mara ya mwisho sasa!