Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Gambo acha ngonjera;
1. Kwanza hukuondoka kwenye kikao, bali ulikimbia baada ya kusikia Makonda anakuja. Na ulisahau baadhi ya vitu vyako ukumbini ikabidi mtu mmoja akukimbizie kwenye gari. Kikao cha bajeti, Mbunge anapaswa kuhudhuria mwanzo hadi mwisho kwa mujibu wa kanuni. Sio unakimbia afu unajitetea ulikua na majukumu mengine. Yapi?
2. Unadai Makonda katengeneza wapambe. Hivi umesahau wewe ndiye mwasisi wa kutengeneza wapambe? Umesahau ulimwahidi JPM utamletea wapambe pale Sheikh Amri Abeid, lakini wakaingia mitini? JPM akakuuliza watu wako siwaoni? Ukajiumauma, akakutukana, Pumbavu mbele ya mic. Umesahau? Nitakuwekea ile video ikukumbushe.
3. Unasema wewe ndio Mbunge kwahiyo, uachwe ufanye kazi yako na muda ukifika wanaotaka hiyo nafasi wajitokeze? Hivi wewe ukiwa RC ulimwacha Lema afanye kazi yake? Wewe si ulikua unamwandama Lema kwenye kila jambo mpaka ukamfungulia kesi ili ashindwe kufanya kazi yake? Leo karma imerudi kwako unatia huruma? Tulia unyolewe.
4. Halafu hioo eneo la stand huko Murriet umeambiwa taja wahusika waliotaka kula hizo milioni 200 ili TAKKURU iwachukulie hatua. Hutaji, unazunguka tu. Kusema kuna hela zilitaka kuliwa lakini hutaji waliotaka kula, inafanya madai yako kuonekana ni majungu tu.
5. Huo ubunge ulipewa kama zawadi kwahiyo jiandae kisaikolojia kufungasha virago. Unajua wazi kwamba hukuwa na ubavu wowote wa kushindana na Lema 2020. Alikugaragaza, lakini ukasaidiwa na dola. Hata Leo Lema akisimama Arusha huwezi kumshinda. Sasa this time tunakula "popcorn" tukitizama mnavyotifuana wenyewe kwa wenyewe. Na kadri unavyotoa mlio ndivyo wanavyozidi kukabia juu. Karma haikuachi. Msumari hutokea palepale ulipoingilia. Karaghabao.!