Huyu hapa mbeba maono wa Simba SC kuelekea msimu ujao 2025/26

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
4,095
Reaction score
13,016
Wakuu,
Ngungu kama ngungu, maono ya simba sc yamebebwa na huyu mwamba, ukimuangalia tu kwa jicho la kawaida unaona kabisa ni tapeli pamoja na jopo lake lote.

Nadiriki kusema, kama huyu mwamba pamoja na jopo lake hawatong’atuka simba sc, ni vilio tena. Kwanza wapinzani wao wanawamudu.

Kugungwa mara tano mfululizo na watani zao, wakulaumiwa ni wao mikakati mibovu, usajili usikizi viwango, janja janja nyingi, wakiwahadaa mashabiki zao kwa caf ranking.

Mashabiki wamechoka sasa, miaka minne ya ubora wa simba, wakiwafunga yanga mara tatu pekee, tena siyo mfululizo. Kwenye ligi mara moja na kombe la fa mara mbili. Tofauti na hapo ni vipigo na sare.

Mashabiki wanajiuliza misimu minne wanajenga timu? Ili hali kila mwisho wa msimu wanaacha rundo la wachezaji? Upigaji kupitia usajili, kuna watu wananeemeka pale, hawana haja na vikombe.

Wanasimba shikikieni hapo hapo, mkilegeza mtakandwa tena mara ya saba mfululizo.



 
Huyu huyu aliyemkodisha Manzoki kuja kumsaidia kufanya kampeni!
 
Tufanye kazi Taifa letu ni Masikini sana.

Huyo amewekwa simba makusudi kabisa na Kiongozi mmoja Mkubwa wa Nchi.
Na huyo kiongozi aliwambia Ole wako Ujiuzuru (Ung'atuke).

Anatimiza Vema majukumu aliyopewa na Kiongozi wa selikali.
 
Ngungu Boy! Wapi Manzoki? 😀
 
Nimeipenda hiyo picha ya Mangungu.
 
Leo nataka niwaumize mashabiki wa simba.
Kama kila kitu kingekaa sawa wachezaji wafuatao Leo wangekuwa Simba.

1. Khalid Aucho.
2. Azizi Ki.
3. Mudahir yahya.
4. Bakari Nondo mwamnyeto.
5. Pakome Zizu.
6. Max Nzengeli.

Yanga wanatembea na Copy ya simba kwenye kila kitu.
Uwekezaji.
Matamasha.
Uozngozi.
Usajili nk
Kila kitu huwa wanacopy msimbazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…