Huyu hapa ng’ombe anayekamuliwa lita 45

Huyu hapa ng’ombe anayekamuliwa lita 45

KILIMO_MAGAZINE

New Member
Joined
Mar 27, 2022
Posts
3
Reaction score
3
TAZAMA MAAJABU YA NGOMBE AINA YA FRISHIAN F1 HII NI SABABU TOSHA YA KUFANYA UFUGE KILICHO BORA

Hawa ni ng'ombe wa mziwa aina ya frisian hapo tumepost f1 na f2 wanapatikana Uwezo wao wa kutoa maziwa ni unalingana na ubora wa vinasaba(genes) vyao. Frishiani F1 anauwezo wa kutoa lita 45 kwa ng'ombe mmoja kwa siku Frishiani F2 anauwezo wa kutoa lita 30-35 kwa siku Cross zingine za frieshiani zinatia lita 10, 15, 18, 20 hadi 25 kwa siku Ng’ombe aina ya freshiani ni rahisi kumtambua kutokana na kuwa na rangi nyeusi na nyeupe, na ni ng’ombe wenye uzalishaji bora wa maziwa.

Wanyama hawa ni wakubwa na pia wanaweza kuwa na mabaka meupe na meusi. Ikiwa watalishwa vizuri, freshian aliyefikia umri wa kukomaa huwa na uzito wa hadi kilogramu 550 na urefu wa sentimeta 150 kutoka begani. Mtamba huweza kupandwa, akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi mitano huku akiwa na uzito wa kilogramu 360. Wakati baadhi ya ng’ombe wakiwa na uwezo wa kuishi kwa muda mrefu, uwezo wa kawaida wa kuishi kwa Freshiani ni miaka sita.

Hata hivyo, aina hii ya ng’ombe ni wazalishaji wazuri wa maziwa ambao huweza kuzalisha kilogramu 7800 kwa wastani kwa muda wa siku 360 yakiwa na kiwango cha chini cha mafuta ikilinganishwa na aina nyingine ya ng’ombe. Aidha, aina hii ya ng’ombe huhitaji ulishaji mkubwa hivyo hushauriwa kwa wafugaji wenye uhakika wa kuwa na lishe bora na ya kutosha kwa mwaka mzima

(1) Tunao mitamba ambao awajapandwa ila waweza pandwa mda wowote bei ni kuanzia Tsh 1800000 adi 2000000 inategemea na mtamba wenyewe
(2) Pia mtamba mwenye mimba kuanzia miezi mitatu (3) adi miezi sita (6) ni Tsh2000000 adi 2500000

(3) PIA tunao ng'ombe walio zaa mara moja mara mbili na mara tatu ambao wanakamuliwa maziwa kuanizia liter 16 adi 22 inategemea na ng'ombe mwenyewe bei zao ni kuanizia Tsh 2300000 adi 2600000

(4) Na pia kwa wale wanao itaji ndama madume pamoja na majike wanapatikana kuanzia umri wa miezi minne adi sita kwa bei kuanzia Tsh 750000 adi 850000

KARIBU SANA UPATE NG'OMBE WAZURI KWA UZALISHAJI

wasiliana nasi kwa simu namba
0765849849
FB_IMG_1675505688754.jpg
FB_IMG_1674932937212.jpg
FB_IMG_1674932939810.jpg
FB_IMG_1674719751978.jpg
FB_IMG_1674719586554.jpg
1674681590232.jpg
FB_IMG_1674719566893.jpg
 
Hizo Lita 45 inategemea na mkoa Gani..Lushoto, iringa, kitulo, busokelo,makete, Moshi na maeneo mengine yenye Hali ya hewa ya ubaridi ndo unaweza pata hizo Lita, Tena under good management kuanzia lishe Bora, chanjo kwa wakati.
Maeneo kama Dar es salaam, utaishia kupata Lita 10
 
Wanauzwa wapi Hawa nahitaji wawili kama bei itakuwa nzuri
 
Yaani nilitamani saana kuona huyu mtu akijibu maswali anayo ulizwa, ila kama kuna mtu hapa mwenye ujuzi na masuala ya ngombe wa maziwa, anaweza tusaidia uzoefu na jinsi ya kuwapata hao ng'ombe.
 
Yaani nilitamani saana kuona huyu mtu akijibu maswali anayo ulizwa, ila kama kuna mtu hapa mwenye ujuzi na masuala ya ngombe wa maziwa, anaweza tusaidia uzoefu na jinsi ya kuwapata hao ng'ombe.
Mleta mada kaweka namba ya simu mkuu, unaweza kumpigia akakupa maelezo unayohitaji...
 
Ng
Yaani nilitamani saana kuona huyu mtu akijibu maswali anayo ulizwa, ila kama kuna mtu hapa mwenye ujuzi na masuala ya ngombe wa maziwa, anaweza tusaidia uzoefu na jinsi ya kuwapata hao ng'ombe.
Ng'ombe wa maziwa unamtengeneza mwenyew zizin kwako mkuu hao wa kununua kwaTZ kukuuzia mtu ng'ombe wa lita 30+ sio rahis.
 
Kupandisha kwa AI ndio ataanza kupa hao ng'ombe anaowataka taratibu taratibu hadi atafika F4

Huo ndio ukwel kama anatak kuanza kufuga atafute ng'ombe ambaye ameshazaa anauwezo wa kutoa lita ata 5 ndio aanze kupandisha kwa AI
 
Ninao lakin siwauzi, ila changamoto kubwa ni msosi wanakula mnoo
 
Back
Top Bottom